Wale wanaosemaga China wanatupenda hawajui hawa watu vizuri

Hakuna undugu na heshima kati ya tajiri ya masikini, rafiki wa tajiri ni tajiri na rafiki wa masikini ni masikini... ukitaka uwe na urafiki na matajiri na watu wenye uelewa inakupaswa nawe uwe tajiri pamoja na uelewa..

tusilazimishe kuheshimiwa wakati hatuna kitu na hatuna msaada wowote duniani na hatufanyi lolote la maana kuendeleza mataifa yetu zaidi ya kuyabomoa kila siku....

WaAfrica tuache ujuaje tupambane kuijenga Africa kutengeneza heshima kwa vizazi vyetu vya baadaye...tukiendelea kuwa ombaomba na kujipendekeza kwa weupe tutaendelea kudharauliwa na kubaguliwa milele...
 
China ilijengwa kwa jasho na damu kama ilivyojengwa Ulaya na America..... ilifanywa na mababu wa mababu kwa miaka mingi kwa manufaa ya vitukuu na wajukuu zao...

Sasa wewe unatoka tu kwenu huko unakuja kujipendekeza na kufurahia matunda ya mababu zao unataka wakuchekee wakati babu yako na wewe wote wazembe, babu yako hakufanya lolote kwa nchi yenu na wewe mwenyewe hufanya lolote kwa nchi yako zaidi ya tamaa na vitu vya watu ulivyovikuta tayari....

Njia pekee ya dunia kuacha kuidharau Africa ni waAfrica kuijenga Africa yao na kuacha kuombaomba vimisaada kila siku na kuendekeza vinjaa vyetu hivi..... leo hii kila mtu duniani inambagua MwaAfrica, Mchina kaja juzi naye anatubagua baada ya kujiuliza shida nini tunaendeleza lawama kwa dunia.....

WAAFRICA TUFANYA KAZI TUJENGE MATAIFA YETU KWA JASHO NA DAMU TUACHE KULIALIA NA KUDEKADEKA, HAKUNA WAKUTUDEKEZA DUNIANI HAPA, tukasome historia za wenzetu mateso waliyopata kujenga miji yao..
 
Huyo mtoto anaambiwa juu ya ujinga wa WaAfrica pale China na namna tunavyoweza kuwaangamiza wachina...

Nani anauza unga pale China, nani anafanya umalaya pale China...Kuna madada wengi wa KiaAfrica pale China wanazagaa hovyohovyo wakifanya umalaya, kuna vijana wengi wa KiAfrica wamejaa pale wanauza unga na wizi na ujinga mwingi......Kabla ya kuilaumu dunia tujitafakari..
 
Wachina wanafanya kitu sahihi sana kwa upande wao na inabidi wafanye sana, waafrika tuna tabia za ajabu na za kuogofya tuchukulie mfano tu hapa kwetu Tanzania mtu akipenyapenya akabahatika kua askari wa jeshi lolote la serekali utashangaa ghafla anabadilika na kua na kiburi/jeuri hakuna tena mtanzania kama yeye, sasa unajiuliza mlinzi anapataje kiburi na hapo ni kada ya ulinzi hujaingia kada zingine. Ninachotaka kusema waafrika hatupendani sio rahisi mchina kutupenda, tupendane kwanza tuungane kwanza tuone kama kuna mchina atatuchukulia poa
 
Kuna watu wanafikiri kule China tunaheahimiwa kuliko sehemu nyingine Duniani kama US . Huu sio ukweli tofauti ni kwamba kwasababu US vyombo vya habari viko wazi tunasikia matukio mengi lakini wa China ni wabaguzi mara 100 zaidi


Na sis waafrika tunazngua kutwa kuzamia kwny nchi za watu
 
Mchina ni mmoja ya mtu mshenzi sana tulikuwa tu hatuwajui
 
The only way to survive in this world, make sure una pesa. Pesa ndio itaamua heshima yako, huwezi kuwa masikini hapohapo unataka ule pamoja na wakubwa [emoji28][emoji28]
Tunaongelea wachina sio wakubwa
 
Wala siyo hivyo!
Ukiangalia huyo mama anaongea kwa kurefer matukio means kuna sababu iliyompelekea kumfunza dogo hivyo

Tuache kuvamia miji ya watu na kuipamba kwa sifa/tabia mbaya inasababisha kuwaponza wengine na ndicho kilichotokea kwa huyo mama

Hata kwetu huku imekuwa ni kawaida ukiona au ukifanyiwa jambo na minority ya jamii fulani basi inakupeleka uihusishe jamii yote... utasikia "wachaga sitaki hata kuwasikia", "kabila fulani wezi", "watanzania wavivu" nk
 
Kulalamika sikuzote ni ushenzi na inashusha heshima, kwann unalalamikie ujinga, kama wanawaza hvyo waache we fanya yako watuonee gele kimaendeleo,
Waafrica wenyewe ndo tunafanya mpaka watu watuone hvyo, hatujielewi kweli, yani tunallaamika kila kona tunabaguliwa uku ata bara letu wenyewe kuliendeleza na kutawala vizuri hatuwezi, heshima sikuzote haiombwi, heshima ni haki yko kama mtu upande wa pili ataona unajielewa
 
Reactions: R.K
Wachina wanafanana tabia na CCM, wako radhi kufanya lolote ili wabakie madarakani lakini utu hawana.
Wewe mmama waga nakuonaga lijinga sana, miaka yako yote utaishi kwa kushangaa matukio na kulalamika, mi si mtu wa chana ila hujui unachopenda, ungejua nisingekudharau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…