Wale wanaotamba "Najua kuacha sijui kuachwa" mara nyingi baadae huwa wasumbufu kwa wapenzi waliowaacha

Wale wanaotamba "Najua kuacha sijui kuachwa" mara nyingi baadae huwa wasumbufu kwa wapenzi waliowaacha

kamba0719

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2018
Posts
804
Reaction score
1,906
Kuna wale wanajionaga mafundi wa mapenzi sababu ya mionekano yao,uzuri au fedha zao wanajiamini kwamba wanajua kuacha hawajui kuacha,ila baadae hujaga kuwa wasumbufu.

Nakumbuka nilikuwa na demu mmoja mzuri, ki ukweli huyu demu alikuwa mzuri Black beauty bonge la figure, halafu mara nyingi alikuwa anapenda kuvaa nguo za vitenge. Kidume nikakomaa nae miezi minne ,mtoto akajaa kumbe huku nyuma alikuwa na ex-wake style yao ilikuwa ya kuachana na kurudiana. Nilikuwa sijui ila kuna siku kuna dogo mmoja hivi akanionyeshea jamaa kwamba ,ndiye aliyekuwa anamiliki goma nikaona poa. Siku ya siku nandikiwa meseji ndefu mbili, zikiambatana na dharau plus kejeli zikahitimisha na ....mimi na yeye basi....amemua kurudiana na mpenzi wake wa zamani.Kwanza sikuamini nikamtafuta kwenye simu akawa hapokei, kufupisha story akaweka picha ya yy na ex wake walio rudiana ,kwenye status plus viemoj vya makopa.Nikasema kweli hapa nishakula kibuti, nikasema wacha nikomae nimtafute niongee nae wapi, ikapita kama wiki nikajipa moyo japo ule mwezi ulikuwa mrefu na mgumu sana. Ila na shukuru baada ya miezi kama mitatu nikawa sawa. Ikapita miezi tisa si akarudi kuomba kurudiana nami,akinipiga mikwala kuja home kufanya vurugu, mara atamfanyia vurugu demu niliyekuwa nae (wakati mimi sina mtu) nk.Nikamvumilia ila nikamwambia ,sijawahi kupiga mwanamke ila siku atakekuja ghetto kufanya vurugu ndipo atanijua mimi ni nani. Naona akawa mpole akaanza kutumia marafii zangu tuyamalize, mimi ndio kabisa sina time nae mpaka sasa hivi anaomba turudiane.

Wapili huyu jamaa ni mwanagu na kumbuka kipindi nipo A-Level kuna demu nilikuwa na mkubali, ila ndio hivyo mzigo sina,pamba zenyewe za Karume.Kuna mwana mmoja akaisogeza pale akawa analimiliki lile toto. Huyu jamaa demu alikuwa hamtreat vizuri kabisa, anaenda club anarudi na mimalaya (mziuri),siku nyingine anampiga. Imeenda jamaa akamwacha demu ila wakawa ile wanaachana wana rudiana. Baadae yule akachoka akapata mwana mmoja, mtaa wa pili yule jamaa kusikia alienda kumfanyia fujo mwana na mikwala mingi wakati kwa mujibu wa demu washaachana na jamaa. Yule mwana akamua kumuacha demu maana ilikuwa kero kwake. Sasa ukapita mda kidogo,akaja kumpata mtu yupo vizuri kiuchumi mwanzo jamaa akataka kumfanyia fujo huyo jamaa mpya,ila ndio hivyo jamaa kamawambia akithubutu atamweka ndani ,mwana akawa mpole antizama show.Demu mpaka sasa kazalishwa watoto wawili na huyo jamaa yake mpya na anazidi kunawili.

Hii ya mwisho ndio sometimes huwaga na chelka nikikumbuka visa vyao. Kuna mama mmoja yy aliachwa na aliyekuwa mme mumewe kwa zaidi ya miaka kama 11 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja.
Jamaa alienda akaoa mke mwengine baadae tena wakaachana, akarudi kwa huyu mke wake aliye zaa nae ,yule mama kipindi hiko hakuwa na mahusiano na wala alikuwa hataki mahusiano. Mwamba si akarudi bembeleza wapi,akaamua kuanza kumfuatilia yule mama nyendo zake, akiona kasimama na mwanaume yule mwanaume lazima baadae amtafute amfanyie fujo, siku nyingine anakuja ofisini kwake na kujitapa kwamba "....mimi ndiye mmewe.....baba watoto wake....".Yule mama akawaambia ndugu zake fujo anazo fanyiwa na baba watoto wake,kuna kaka yake akamfuata yule mzee na kumwambia hasithubutu kumsumbua dada yake ,yule mzee akawa mpole ila still bado akawa anamsumbua. Sasa yule mmama akapata mtu mpya, sasa siku nyingine yule mzee akawa analala kwa yule mmama.Hapo sasa ndipo nilipo muona yule mmewe ni kituko, alikiwa anavizia usiku akimwona yule mzee kaja kulala kwa yule mmama,anarusha mawe juu ya mabati ya nyumba aliyopanga yule mmama, halafu anakimbia 🤣🤣🤣🤣🤣.Yaani alikuwa kama chizi.

Sasa na jiuliza nyie mabingwa wa kuacha,hivi mnakuwa mnaona kitu gani kipya kwa watu mliowacha kwa visa,kejeli na dharau na kutaka kurudiana nao.
 
Kiburi tu cha kishamba..

Unakuta mtu kamuacha mwenzie then mwenzie kaumia mpaka kampotezea kaanza Maisha mapya..Baadae unakuja sikia anamtaja kila kona
 
Ahahahahaaa umenikumbusha mbal sana siku moja dem wangu alinambia tuachane baada ya kupishana kaul kdg me nkasepa zangu ila siku hio nakumbuka tulichat sana mara anitukane mara hvi mara vile nkaona anavyonitukana nismjib lolote maana hakuna kitu kinauma kama unamchokoza mtu alaf yeye nikama hana muda bas bhn hio cku ikapta baada ya siku kma 3 hv naona anatuma msg hata kama tumeachana ila sio kuwa kmy kiasi hicho kumbe alitaka tu tuendelee mpaka now bad niko nae
 
Ahahahahaaa umenikumbusha mbal sana siku moja dem wangu alinambia tuachane baada ya kupishana kaul kdg me nkasepa zangu ila siku hio nakumbuka tulichat sana mara anitukane mara hvi mara vile nkaona anavyonitukana nismjib lolote maana hakuna kitu kinauma kama unamchokoza mtu alaf yeye nikama hana muda bas bhn hio cku ikapta baada ya siku kma 3 hv naona anatuma msg hata kama tumeachana ila sio kuwa kmy kiasi hicho kumbe alitaka tu tuendelee mpaka now bad niko nae
Ni vyema ulivyo mkazia japokiwa kuna baadhi ya makauzu wengine hapo ndio nitolee.
 
Back
Top Bottom