Wale wanyapara wameacha zile tabia zao

madala mujipa

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Posts
1,417
Reaction score
862
salaam wana jf
ndugu zangu jana nimetoka mahakamani na natakiwa kurudi siku ya jumanne kila nionavyo nina dalili ya kuingia gerezani

Kisa nilimpiga muuza samaki, nilikuwa nipo ndani nikasikia neno tajiri kama mara nne nje ya nyumba,nikasikia watoto wakijibu tajiri yupo ndani ,baba pia yupo nikamuuliza wife mbona hujibu kumbe unaitwa wewe akaniambia aah nawe hujui watoto,mara namsikia muuza samaki anasema nitarudi baadae

nikamuuliza wife hebu nenda kamsikilize akaniambia aah muache mimi nikamlazimisha wife akatoka nikamchungulia dirishani nasikia kidogo kwa sauti ya chini ukiniita ukiona siitiki ujue mzee yupo muuza samaki anamjibu sasa akiwepo na sisi hatuli wala hatunywi nikamuona wife kama amefadhaika

Nikasikia watoto nao tajirii leo hunywi chai au huna vitumbua na samaki leo huwachi kengele ya hatari ikagonga nikatoka nje sikuuliza nikakata nilimpiga mikia ya taa mingi na kumjeruhi jicho la kushoto na mguu

akaenda kushtaki nikapelekwa kituoni then mahakamani ndugu zangu naona kesi imekaa vibaya nataka ushauri je nikimbie msala au, na kule jela naogopa nyapara nasikia wana tabia zao fulani

asanteni
 
Hahaha apole sana mwanaume wasiwasi ndo akili siku hizi hayo mambo hamna kule ni wewe kujilegeza na kutaka slope ndo itakucost.halafu mwanume lazima uwe ngangali bwana
 
kesi uliyo nayo ni yakawaida.ila jela pako sawa tu.hakuna shida wala mizunguo kama tunayo yaona kwa bashitw
 
Pole sana mkuu, ila nakuusia kuwa; Wanaume hawapigani wala hawawapigi watu. Wivu wako wa kijinga ndo huo unakupeleka ka miaka 2 hivi. Ukirudi aliyekuamshia wivu utamkuta anamnyoyesha mtoto wa miezi ka 4 hivi ndo utashika adab.
Mwanamke usimwonee wivu, mtunze atatulia tu ndani wauza samaki watapata wapi nafasi ya kuhonga samaki tena wabichi?? Ulipokuwa unakuja ukakuta samaki maziwa ulidhani hiyo shs 2000 yako ndo imekununulia vyote hivyo?? Na ugali mara useme,Ongeza sijashiba miyeee. Mama anapanua miguu ili ushibe. Nenda Segerea uwakute wanaume
 
Hahaha apole sana mwanaume wasiwasi ndo akili siku hizi hayo mambo hamna kule ni wewe kujilegeza na kutaka slope ndo itakucost.halafu mwanume lazima uwe ngangali bwana
dah mkuu si nawacha mkwanja kawa
 
mke unamuachia muuza samaki na atahamia kabisa.

vitu kama hivyo unapaswa kuwa kuweka mtego umkute ndani ili upatikane ushahidi wa kutosha
sawa mkuu lakini suala la hasira halina subra
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…