madala mujipa
JF-Expert Member
- Feb 23, 2017
- 1,417
- 862
salaam wana jf
ndugu zangu jana nimetoka mahakamani na natakiwa kurudi siku ya jumanne kila nionavyo nina dalili ya kuingia gerezani
Kisa nilimpiga muuza samaki, nilikuwa nipo ndani nikasikia neno tajiri kama mara nne nje ya nyumba,nikasikia watoto wakijibu tajiri yupo ndani ,baba pia yupo nikamuuliza wife mbona hujibu kumbe unaitwa wewe akaniambia aah nawe hujui watoto,mara namsikia muuza samaki anasema nitarudi baadae
nikamuuliza wife hebu nenda kamsikilize akaniambia aah muache mimi nikamlazimisha wife akatoka nikamchungulia dirishani nasikia kidogo kwa sauti ya chini ukiniita ukiona siitiki ujue mzee yupo muuza samaki anamjibu sasa akiwepo na sisi hatuli wala hatunywi nikamuona wife kama amefadhaika
Nikasikia watoto nao tajirii leo hunywi chai au huna vitumbua na samaki leo huwachi kengele ya hatari ikagonga nikatoka nje sikuuliza nikakata nilimpiga mikia ya taa mingi na kumjeruhi jicho la kushoto na mguu
akaenda kushtaki nikapelekwa kituoni then mahakamani ndugu zangu naona kesi imekaa vibaya nataka ushauri je nikimbie msala au, na kule jela naogopa nyapara nasikia wana tabia zao fulani
asanteni