Uongozi wa Simba SC ubadilike na uache nao kufanya 'Uswahili' Kwetu Sisi Mashabiki.
Sihitaji kumtizama Mchezaji kwa dakika 90 au Mechi 3 au 5 ila Kwangu Mimi GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE nikimuona tu Mchezaji kwa dakika 5 mpakae 15 zinatosha kujua Uwezo wake.
Namheshimu sana Kiungo Shiboub ila kwa sasa na anavyocheza nitaulamu mno Uongozi wa Simba SC ukimsajili kwani Simba SC ya sasa ina Viungo wazuri wa Kumzidi.
Huyu Mchezaji Moukoro Tenena ( Ivory Coast ) ndiyo bure ( hovyo ) kabisa kwani nae anazidiwa Vitu vingi na Mzawa Yusuph Mhilu.
Poti wangu Crescetius Magori najua 'unanifolo' na kunisoma sana hapa JamiiForums tafadhali achaneni na Shiboub na huyo Moukoro bali mwambie Mo aache Ubahili ( Ulugume ) wake na atusajilie Majembe ya maana siyo Vituko hivi.