Wale wote 'mnaomtetea' Haji Manara na 'Upuuzi' na 'Unafiki' wake popote pale mlipo naomba mnijibu haya Maswali yangu Kwenu

Wale wote 'mnaomtetea' Haji Manara na 'Upuuzi' na 'Unafiki' wake popote pale mlipo naomba mnijibu haya Maswali yangu Kwenu

1. Je, Kisheria baada ya jana Haji Manara kuitaja Kampuni ya Azam akiihusisha kuwa na Vita ya Chuki na Kampuni za Mohammed Dewji yuko salama kama aliyeguswa akitaka Kumshtaki?

2. Je, kati ya aliyekuwa CEO Magori ambaye hakuwa kumpa Mkataba wowote Haji Manara na CEO Barbara ambaye kwa mwaka mzima alimpa Mkataba wa Milioni 4 kwa Mwezi ila akawa hataki nani ni Mzuri Kwake na nani alikuwa hamthamini?

3. Katika Sheria za Ajira na Miiko ya Kazi moja wapo ikiwa ni Kutokutoa Siri za Taasisi / Kampuni hivyo basi je, leo hii kwa Mambo ya Siri (ya ndani ya Menejimenti) ya Klabu aliyoyasema Haji Manara Simba SC ikiamua Kumshtaki Mahakamani atakuwa salama?

4. Je, kati ya Haji Manara ambaye amekiri kuwa amekaa Simba SC miaka Sita (6) bila kuwa na Mkataba huku akiridhika na Hali hiyo na Klabu ya Simba ambayo haikumpa huo Mkataba ni nani ni Mjinga (Ngumbaru) na Mpumbavu (Popoma ) hasa?

5. Haji Manara mara kwa mara amekuwa akisikika akiwadhihaki na akiwadharau Waandishi wa Habari akiwaita Takataka je, Haji Manara jana kaongea na Waandishi wa Habari Takataka au Waandishi wa Habari wa Kimataifa?

6. Je, ni kweli kuwa Haji Manara ndiyo Kainyanyua Simba SC Kiumaarufu tokea ianzishwe mwaka 1936 na kwamba Yeye ndiyo ana Thamani Kubwa kuliko Wazee wote wa Simba SC ambao tena wameifia Simba kwa kujitoa Mhanga ili aikute Simba SC hii aliyoikuta Yeye? Mfano Mzee Bamchawi na Wengineo.

7. Je, kwa tabia ya Umbea na Kuropoka aliyonayo Haji Manara mpaka ya Kutoa Siri za Taasisi na Kampuni unadhani kuna Vilabu vingine au Kampuni ( Corporates ) zingine leo hii zitathubutu kutaka Kufanya Kazi nae?

Ninayasubiri sana tu Majibu yenu hapa.
Haji anasilimu na kuingia yanga wiki 2 zijazo

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Umenena vema sana mkuu. Nashangaa hata TFF wameuchuna tu.
Haji kama hakuridhika angewaachia wenye timu ama la angefungua jalada.
Sitaki kuamini utopolo leo wamesimama na Manara! Maisha yanaenda kasi sana aiseee! Mo tunajua ndio shida yenu,yaani maskini hapambani amfikie tajiri ila dua zake siku zote ni tajiri afilisike!

Hivi utopolo simba akishuka kiwango kwa kukosa udhamini mtafaidika nini? Uto hamuoni raha siku moja nchi inakuwa na vilabu giants nchini kuanzia kiuchumi hadi uwanjani?

Mfano misri kuna ahly,zamalek,pyramid nk,yaan ninyi mnaanzisha chokochoko simba iporomoke,akili za kijinga kabisa! Utopolo na wapenda mpira tunapaswa kukemea alichokifanya manara wadhamini au wawekezaji wataogopa kuwekeza ktk mpira wetu!
 
Mkuu unaona kinachoendelea Barcelona ubovu wa management ndio umewapeleka pale
Yes nauona ndomaana ata last season wamefanya vibaya sana kwenye mashindano yote hila bado Simba ajapitia hizo hekaheka toka Mo apewe team so far team inapelekwa vizuri tu makombe muhimu ya ndani wanachukua kimataifa wanafanya poa sasa kuna ubaya gani boss akirudisha chenchi zake?
 
Back
Top Bottom