Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

eBay na Amazon vipi kwenye utumaji wa electronics? In terms of cost na muda wa kusubiri

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu haya mambo ya kuagiza nilianzia eBay then nikahamia mazima aliexpress kutokana na unafuu wa bei maana vitu vingi kutoka China kule vinauzwa bei kuliko Aliexpress.
Upande was Amazon sina uzoefu nao.

Shipping EBay ni kama ifuatavyo:-
1.FedEx na DHL:
Siku 3-8

2. UPS:
siku 4-8

3. USPS (First Class Mail Int'l): Siku 14-24 kutokea USA..

4. USPS (Priority Mail Express Int'l):
siku 7-14 kutokea USA..

5. Royal Mail (International Signed):
siku 8-12

6. Royal Mail (Small Packets):

siku 14.....

7. Standard Int'l:


Siku 9-28 kutokea USA, 14-35 kutokea Asia, na 5-14 kutokea Europe..

8. Economy Int'l:

Siku 21-45 kutokea China..

9. Hong Kong Post Airmail:

Siku 15-60 kutokea China

NB:- Namba 1 Shipping cost ni kubwa pia jiandae na rungu la watu wa TRA.
Namba 5 na 6 Ndio wana Shipping cost rahisi na parcel yako inafika ndani ya siku 14 kama hakuna any delay.
Namba 7-9 Mara nyingi huwa Free shipping au hela ndogo sana ila ndio mambo ya kusubiri wakati mwingine hadi Isiku 40 au 60
 
Unaweza kunielekeza jinsi ya kuagiza hii simu next week nifanye utaratibu
Kwanza: Jisajili kwenye website husika AliExpress, Gearbest, LightInTheBox, eBay nk . Utajaza taarifa zako zote muhimu.

Pili: Unatakiwa kujaza shipping address hapa wengi tunatumia postal address kwa sababu ya unafuu.

Tatu: Unatakiwa kuwa na njia ya malipo utakayotumia kulipia, utajaza taarifa za malipo kama ni kwa Debit card, Credit card, Prepaid card, Virtual card ( VISA or MasterCard branded), paypal, wire transfer, western union, nk.

Mwisho: Mzigo utauchukua ofisi ya posta. Unaweza kulipa kodi au usilipie.
 
Ila kama ndio unaanza,... Anza kuagiza vitu vyenye thamani ndogo Mf: Earphone, SD Card, Flash Drive, etc kupata uzoefu zaidi. Ili ukitaka kuagiza mzigo wenye thamani unakuwa hauna hofu na unachokifanya.
Asante mkuu
 
Asante sana
 

Pia zingatia kama ndio unaanzia anza na order ya items zenye bei ndogo ilikupata uzoefu.

Sent by SangaweJr
 
kwenye upande wa njia ya malipo unaweza kutumia master card ya M-pesa kulipa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…