Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Ngoja tuone mkuu ila ni phone case tu kwa majaribio maana ndo mara ya kwanza kuagiza mzigo online

Hata hivyo kuna jamaa wengine nimewafuatilia juzi wana ofisi Kariakoo, wana maagent kule China
chini ya kilo tano wanatoza 10 USD nimepanga ngwe ijayo niwatumie hao kuniletea simu ya wife
Inamaanisha kwamba anategemea zaidi namba ya simu yaani mzigo Ukifika unabaki posta Kuu na atapigiwa simu kupita namba yake aliyoisajili aliexpress.
 
Ndio inatosha ila Hata ukiwa na sanduku mzigo hauwekwi sandukuni kl, kwenye sanduku wanaweka kikaratasi tu chenye code fulani

Muhusika wa sanduku atakiwasilisha hicho kikaratasi mapokezi na atakabidhiwa mzigo wake kama ni simu au spika n.k

Mimi sina Sanduku nimeweka namba ya simu tu, watanipigia kava langu la simu likishawasili, track namba inasoma mzigo utawasili Jumanne ya wiki ijayo
Kwa hiyo mzigo ukifika wanaweka kwenye sanduku lako?
Mzigo kama simu unatosha kwenye kile kibox?
 
Ina maana umeandika physical address? Na namba ya simu sio?
 
20% kiasi cha kawaida sana. Ukitumia DHL ni zaidi ya hapo.
20% ni kimbembe Kaka iwapo umeagizia mtu mzigo wa laki 5 ina maana laki nzima itakutoka hapo!!
Shida ni kwamba jamaa ushamwambia gharama yako ni 30,000 hujampanga kuhusu kodi Mbona utakuwa mtafutano.
Cha muhimu tusubiri wadau wengine walete feedback tujue mapema.
 
20% no kimbembe Kaka iwapo umeagizia mtu mzigo wa laki 5 ina maana laki nzima itakutoka hapo!!
Shida ni kwamba jamaa ushamwambia gharama yako ni 30,000 hujampanga kuhusu kodi Mbona utakuwa mtafutano.
Mhhh! Hapo pagumu, lakini mara nyingi kwenye invoice hawaandiki hiyo laki tano yote, na kodi inakadiriwa kutokana na invoice ilivyoandikwa.
Juzi nimetoka kuchukua items tano, lakini sikulipia VAT wala customs duty. "Tulipe kodi kwa maendeleo ya Taifa letu"
 
Yaaan! Ni kisanga na robo. Iliwai kunikuta hii ila mteja alinielewa akalipia customs duty na tulitumia DHL ya HK kuleta mzigo. Mie nilikuwa nimezoea ile DHL ambayo nikitumiwa mizigo huwa sichajiwi na mamlaka ya mapato naletewa mzigo hadi mlangoni.
 
Shida wale jamaa wakati mwingine wanakadiria kivyao vyao
 
Watu wa tecno tayari wamesharoga maana Xiaomi tumezidi Tambo na familia inazidi kupanuka!!
Kama ni kweli 20% Itakuwa bora uchukue tu pale kwa muhindi kuliko kuisotea kivile
 
UPDATE:
Kwa sasa ukiagiza simu kwa Posta ni lazima ulipie Kodi hata kama hujatumia DHL.
TRA wanafungua mizigo kuhakiki kila kitu,kodi ni kutegemea na gharama ya simu
Ebu tuambie,... Uliagiza mzigo wa bei gani na ukatozwa kodi kiasi gani kama hautojali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…