Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Hivi kwanini hawa kina tigo wasiingie makubaliano na xiaomi kutuletea hizi simu za kijanja badala yake wanawakumbatia tecno wherever?
 
Nimeagiza hii kwa majaribio
Hivi posta wanakupigia au kukutumia Text mzigo ukifika,maana kazini kuna kelele mda wote.
 
Hivi kwanini hawa kina tigo wasiingie makubaliano na xiaomi kutuletea hizi simu za kijanja badala yake wanawakumbatia tecno wherever?
Kijana hawa watanzania wengi wao hawana roho kama za msukuma mie ngosha ,Chief Mkwawa na wengine.
Mimi sio mjuzi wa tekinolojia ila kitu kikiwa kizuri najua .Iko hivi nilipoona tu kua xiaomi ni wazuri nikafungua uzi.faida ya huu uzi ni kubwa na kila mtumiaji wa xiaomi anajivunia uzi huu.
Leo hii ukifanya research utabaini 90 perc ya watumishi wa tigo hawatumii ni tekno hiyo.Wanatumia brand zingine kali tu .
Kizuri kuleni na wenzenu .Tigo leteni simu nzuri tena muziuze kwa mfumo wa malipo ya awamu awamu .
Tchao
 
Wakuu hizi ofisi zetu nyingi hazifanyi kazi kama inavyotakiwa. Mzigo ukifika inabidi wakujulishe wao ukachukue, sasa kwenda kwa kubahatisha sio sawa. Naupongeza sana uongozi wa posta Dom mzigo ukifika Dar siku yake ya pili upo Dom tayari kwa delivery na wanakutaarifu kwa kukupigia simu au ujumbe mfupi wa maneno.
Sahihi maana anaweza kukaa hata mwezi kusubiri hiyo sms
 
To be honest me sio mtumiaji wa Xiaomi ila nazipenda kwa quality yake respect with worthy for money na nilizijulia kupitia hii thread yako na kuanza kuzifuatilia till now...ulifanya jambo zuri kuwatoa watu wengi gizani kwa hili, I appriciate it.
 
Hiyo bado haijaingia sokoni rasmi, kuwa mpole
natumia red me note 7 pro....inanizumbua sana kuunga mobile internet, ila kwa wifi napata vzuri kbisa.... Nimebadili apn zote nk lakini sijafanikiwa naomba msaada wakuu
 
Hiyo bado haijaingia sokoni rasmi, kuwa mpole
Kuna miaka ya nyuma nilipewa zawadi toleo fulani la ZTE Blade kitu kilikuwa Bomba kimuonekano ila ilikuwa I nasoma 2g tu kwa maana haikuwa na band zetu hizi za 3g so ikabidi niiyeyushe tu kwa hasara.
Ila xiaomi sidhani kama tatizo litakuwa kama hili.
Labda mleta shida mwenyewe ndio mawenge.
 
Hata uongozi wa posta nachingwea tena
Mwambie aje achukue laki na redmi 7 mpya kwani kuunga wifi kitu ganibwana
 
Hivi kwanini hawa kina tigo wasiingie makubaliano na xiaomi kutuletea hizi simu za kijanja badala yake wanawakumbatia tecno wherever?
Mimi nadhani malengo ya kampuni yenyewe, wao walianza kuuza through online, kwa sasa ndio wameanza kufungua Physical store baadhi ya nchi, natumai watafika nchini siku moja, maana kampuni ya Xiaomi inakuwa kwa kasi ya kiwango cha SGR
 
Duuu xiaomi anajua hapa naona rice cooker lenye wifi yaani msosi ukiiva tu kitu kinakupa taarifa kupitia downloaded
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…