Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Hata Mimi nilichukua kwa huyo Jamaa wakuitwa Kashasha...nilikua Na mzuka wa kutumia hii Note 7 GB 32 , kuagiza nikaona kuchelewa. !
Mkuu nilichukua contact hapo kwenye risiti nimepata redmi note 7 shukran Sana.
 
nilikosea mkuu ni 64gb kwa huyu huyu mi france store. tena kwa kuongezea huyo seller yupo fasta sana
 
Kwa wanaoagiza simu jaribuni kucheki na simu za oppo (Realme) wanasimu nzuri kuliko hata xiaomi na bei yao iko vizuri. Simu kama realme x, realme 3 pro zina chipset nzuri kuliko hata hizo note 7, zina fast charging (VOOC) na kama realme x ina amoled display na under display fingerprint.
 
Vp mkuu na wewe unatumia hii Realme kama unavyotushauri?
 
Vipi uki compare na bei zake kama ulizozifananisha Mfano Realme X ma note 7 ni kosa kabisa jaribu ifananisha Realme x na k20 pro,upatikanaji wake ni friendly? naamini pia hata Mi ana simu yenye amoled na fingerprint ya kioo kwa bei reasonable pia kuliko oppo bado Xiaomi ni mkombozi kibongobongo Mkuu.
 
Duuuh sikuelewi mkuu kwa hiyo hio realme ni nzuri kuliko show me ? Kweli kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…