Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Jamani Redmi note 10 5G yangu imezingua vibration, imeanza ghafla tu juzi. Hua nina tendency ya kutopenda kuweka ringing tone, mara nyingi hua napenda kuweka vibration kote hadi kwenye notifications. Sasa ghafla juzi natoa simu mfukoni nakuta missed calls 63 nikashangaa sijaona kabisa simu ikivibrate. Nijaribu kurestart lakini Iko vile vile, nimefanya hadi kuchek tutorials YouTube hadi jinsi ya kufanya vibration test inagoma. Naomba Masada au kama kuna mtu amewahi experience tatizo kama langu. Nawasilisha...!!!
 
Mkuu Chief-Mkwawa vipi kuhusu network kwa tz, haiwezi sumbua, hasa hii ya chinese version.

Pia vipi kuhusu lugha na google playstore, itakuwepo?
 
Mkuu Chief-Mkwawa vipi kuhusu network kwa tz, haiwezi sumbua, hasa hii ya chinese version.

Pia vipi kuhusu lugha na google playstore, itakuwepo?
Simu hizo hizo zinauzwa Global mkuu kwa jina jengine cha muhimu angalia tu band kabla huja nunua Gsmarena.

Mfano Turbo 3 haina band 7 na 20 ina maana Halotel na Tigo mikoani hupati 4G ila Voda, Airtel, TTCL na Tigo mjini unapata 4G, 5G inapiga kote na 3G.

Playstore unaweka mwenyewe na lugha unaweza badili kwenda kingereza ila app za kichina itabidi manual uzitoe.
 
Kwenye hyper os kiongozi app asilimia 99 zinatoka zote bila shida ni single click tu kitu kimetoka
 
Asante sana kiongozi, ugumu upo kwenye jinsi ya kuangalia band, na band gani ni za simu gani, kwa sisi tusiojua mambo ya mawasiliano.
 
Asante sana kiongozi, ugumu upo kwenye jinsi ya kuangalia band, na band gani ni za simu gani, kwa sisi tusiojua mambo ya mawasiliano.
Gsmarena ni rahisi kuangalia mkuu

B3 aka 1800mhz (Voda, Airtel, TTCL na Tigo mjini)
B7 aka 2700mhz (Halotel)
B20 aka 800mhz ( TIGO mikoani na smile)
B40 aka 2300mhz TTCL na roaming mitandao mingine.
 
Asante sana kiongozi, ugumu upo kwenye jinsi ya kuangalia band, na band gani ni za simu gani, kwa sisi tusiojua mambo ya mawasiliano.
Hii simu redmi turbo 3 tayari naitumia toka mwezi wa pili, natumia mtandao wa airtel na tigo, sijapata usumbufu wowote, sehemu nilipo airtel haina 5G ila tigo napata 5G, nimejaribu Vada inakamata 5G, sijajaribu halotel bado.
 
View attachment 3371953
5G wote Tanzania ni band moja? Kama hupo mjini unaweza kutest Tigo 4G?
 
Unaweza niwekea link ya supplier? Na kamuni uliyotumia kusafirisha!
I just found this on AliExpress:
TZS1,387,561.30 | Xiaomi Redmi Turbo 3 5G 6.67” 1.5K 2712*1220 Display Snapdragon 8s Gen 3 50MP+20MP Camera 90W 5000mAh China Rom
Lina bei gani hilo jiwe.

Angalizo! Hizi simu ni Chinese version, na kwasasa uwezekano wa ku unlock bootloader na kuweka globe rom haupo, labda uchukue used ndio utapata tayari wameweka globe rom.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…