huwa apps za google zinaendana na version unayotumia, hata unapoeka custom rom huwezi ukainstall google apps yoyote ile inabidi ueke husika ya version yako. mfano una rom lolipop huwezi install google apps za kitkat utegemee zifanye kazi, zitaload siku nzima.
hapo fanya hivi.
1. install google apps kupitia hio installer, hakikisha app zote zimeingia.
2. by default xiaomi inablock kudownload vitu na mobile data, hivyo hakikisha kila app unairuhusu idownload usibakishe viporo, au ili kuwa salama zaidi tumia wifi ukirun hio google installer.
3. zikimaliza kuingia apps zote fungua store, ikiwa inaload tu download manuall playstore na play service ureplace hizo.
4. zikiingia hizo app tumia ku update apps nyengine za google ulizoeka mwanzo, kwenye playstore ingia my apps cheki updates, zi update zote.
enjoy simu yako