Autostart inatoa ruhusa kwa apps kuanza kufanyakazi zenyewe pindi unapowasha tu simu yako.
Faida zake
1.inakusaidia kupata taarifa kwa haraka zaidi kama message za whatsapp, fb, insta, gmail n.k
2.kupata notifications mbalimbali kama za YouTube, fb, insta, aliexpress n.k
Hasara zake
1.Apps hizo hutumia kiasi kikubwa cha RAM hivyo kufanya simu yako kufanyakazi kwa uzito (inakua slow)
2.Hutumia kiasi kikubwa cha battery hivyo kufanya simu yako istunze chaji kwa muda mrefu
3.Hujaza notifications nyingi katika status bar yako ata zile ambazo hazina umuhimu au husizokua na matumizi nazo
4.Itakula na kumaliza data zako kwa haraka zaidi
Hitimisho
Ni vizuri kama ungechagua Apps chache muhimu ambazo huwa unamatumizi nazo ya kila siku Mf. Whatsapp na Jf uzipe ruhusa hiyo ili kubalance utendaji kazi wa simu yako (hasa kwa wenye RAM ndogo), Na pia kubalance matumizi ya battery life yako (hasa kwa wenye battery yenye capacity ndogo)....Mimi binafsi zijaruhusu Apps zozote zaidi ya (Google Contact Sync) kwasababu ya udogo wa battery yangu na kupata utendajikazi mzuri wa simu vile vile kutunza data zangu zisitumike kwa mahitaji yasiyokua na umuhimu kwangu...Natumaini nimeweza kukuelewesha vizuri.
Sent using
Jamii Forums mobile app