WALEMAVU WALIVYOSAHULIKA NCHI HII.

WALEMAVU WALIVYOSAHULIKA NCHI HII.

KAGAMEE

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
4,457
Reaction score
5,454
Ndugu zangu nmepata wasaa wa kuhudhuria tukio la SPECIAL OLYMPICS TANZANIA linalofanyika hapa jijini Mwanza kitaifa nimejifunza na kuona mengi sana.

Nilijichanganya tu na watumishi wengi wa Uma ili niweze kujua mawili matatu juu ya tukio hilo.Nikataka kujua hili tukio limehusisha watu gani,malengo na namna linavyoendeshwa.

Baada ya kuuliza maswali kadhaa nikaambiwa ni michezo inayohusisha wanafunzi WALEMAVU WA AKILI toka mikoa yote Tanzania na itaendelea huko RWANDA NA UJERUMANI.

Kilichonifanya niguswe kuja na UZI huu ni baada ya kuambiwa mambo ya hovyo yaliyofanya/yanayofanyika katika tukio hilo hapa BWIRU BOYS.

1.Kwanza walemavu na walimu wao wapo mazingira ya hovyo yenye kunguni wengi,Mbu na chakula cha hovyo.Watumishi wanadai kila mkoa ulitoa 3M kwa ajili ya maandalizi lakini WAHUNI WAMEPITA NAZO.

2.Mbaya zaidi Posho ya Maafsa Elimu pamoja na walimu wao hazieleweki.Kuna wengine wanalipwa elfu 5 kwa siku wengine elfu 60 per day.Walimu wengine elfu 5 wengine 60,maafsa Elimu wengine elfu 5 wengne 60.

3.Mashindano hayaeleweki ni ya walemavu au watu wazima maana kuna mikoa imeleta wachezaji ambao siyo walemavu (timu nzima)na wanapeta tu na uongozi upo hapa unakula na kulala.

Baada ya kuelezwa yote hayo nilimtafuta Katibu wa walemavu Taifa bila mafanikio.Niliambiwa ni jamaa mmoja mrefu hivi mwembamba na anavaa miwani huyo ndo kavuruga tukio lote (kapiga hela za kutosha)Aliweka kamati mbalimbali lakini alizivunja baada ya watu kugomea posho kiduchu.

Inasemekana jamaa ni ndugu yake na mkurugenzi wa ELIMU MAALUM TANZANIA ndo maana anapiga pesa hadharani bila hofu.

Naiomba serikali (PCCB) muingilie kati mfatilie tukio hili linaloendelea hapa Mwanza lina uozo mwingi sana linamchafua Mh Raisi kwa kuonesha serikali yake imeshindwa kuzuia wahuni.

Serikali fatilieni pia utendakazi wa MKURUGENZI WA ELIMU MAALUM TANZANIA huu uozo wote unafanyika chini ya utawala wake.

Walemavu hawana wa kuwasemea nchi hii,pesa zinatolewa na serikali zinaishia kwenye matumbo ya watu wachache (laana kubwa sana hii).Kila mtu akiangalia alipo kuna mlemavu amemzunguka,jiulize huyo mtu serikali inamjali?je anapata huduma stahiki?kama HAPANA unamsaidiaje?

OMBI:SERIKALI INGETENGA WIZARA MAALUM YA WALEMAVU.

KAGAMEE
0765746745
MWANZA-TANZANIA.
 
Back
Top Bottom