Walevi wa kahawa 24 hours tukutane hapa

Walevi wa kahawa 24 hours tukutane hapa

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
8,774
Reaction score
13,566
Mi nisema hichi kinywaji kina siri nzito sana, japo watu wengi hawafahamu. Nitatoa sifa chache za hichi kinywaji

Kwanza kabisa katika eneo ambalo wamekaa wanywa kahawa huwa kahawa inamfanya mtu awe na stimu kati ya hizi 2.

Moja kuongea sana hadi story za uwongo,
Na wapili ni kupenda kusikiliza story yani unakua unapata raha furan kusikiliza story yoyote ambayo mwenzio anakusimulia.

Faida zingine ni kama:
- Inaepusha kisukari,
- Inaepusha shinikizo la damu (presha), ila usitumie bila mashariti endapo tayari una tatizo la presha
- Kuchangamsha viungo, vikae tayari kwa kufanya kazi.
- Pia hii kitu inaepusha na kutibu tatizo la viungo vya mwili kufa ganzi.

Faida zingine zitafuata baadae, mtamalizia watumiaji wenzangu.
 
sinywi wala sipendi kahawa japo Hamna harufu naipenda kama Muuza kahawa apite karibu na birika lake

Asee naweza jikuta nimemuita then nimempa offer yeye mwenyewe anywe kikombe kimoja cha kahawa huku nikiendelea

kupata burudani kwenye PUA zangu.
 
Pia hii kitu inaepusha na kutibu tatizo la viungo vya mwili kufa ganzi.
 
Duu basi watu tumetofautiana, yani kahawa pamoja na chai, , , , sizipendi kabisa
 
Kweli maana chai ina viungo zaidi hata ya vitano.
Hujawahi kunywa chai nzuri wewe. Itakuwa umezoea chai ya maji na majani ya chai pekee,lazima ikuboe
 
[QUOTE="Suriya,
Ni kinywaji cha wavivu wa kazi na wapendwa majungu au kuzungumzia habari za watu.

Pia ni kinywaji cha mashushushu wa magogoni na muda mwingi ni kupima joto la kisiasa la wananchi.

Ni kinywaji kinachouzwa kwenye mazingira hatarishi sana kiafya mfano maji hayo hayo huoshwa kikombe hivyo hivyo inakuwa kama mnabadilishana mate 😇😇😇

Ni kinywaji cha wapenda ubishi na vijistory vya kushadadia ali mradi wanavuta muda ili jua lizame.

Kwa ujumla sipendi kahawa za kwenye mabenchi mjini ndo maana huwa sina hata muda wa kukaa hapo.
 
Mkuu kahawa nzuri unaandaa mwenyewe nyumbani MWANAKA
 
Unaniuzia kitu yenye mfumo wa chai halafu huweki sukari?

kama hiyo haitoshi unaamua ku mix na tangawizi kuifanya iwe mbaya zaidi halafu unataka na kesho nikuungishe??
 
Mida hii mizur sana kutafuta nguvu ya kuendelea na kazi.
 
Muda huu mzuri kuandaa kinywaji.
 
Yaani usiombe boss wako dictator afu pia ni addict wa hii kitu, ikifika mida ya kutoka ofisini na umesha-trigger mood yako kwenda kupumzika na familia ye ndo kwanza anachemsha kahawa [emoji4]
 
Back
Top Bottom