Wali spinachi, karoti na mboga mchanganyiko

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji



  • Mchele nusu kilo
  • Karot 1 kubwa (ipare vizuri)
  • Nyanya 3 kubwa
  • Vitunguu maji viwili (ukubwa kiasi)
  • Bizari ya pilau, curry powder, binzari ya njano na mdalasini 1/2 teaspoon kila kimoja
  • Mafuta kiasi
  • Mchanganyiko wa mboga, mfano njegere na mahindi machanga (ila hii sio lazima)
  • Chumvi kiasi
  • Mboga ya spinachi (fungu 1)
  • Saumu na tangawizi ya kusaga (1 teaspoon)


Namna ya kutayarisha

Loweka mchele kwa dakika 20.

Weka mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji hadi karibia kuwa brown

Weka spices zote

Weka tangawizi na saumu

Tia karoti yako uliopara pamoja na vegetable nyengine

Mimina nyanya pamoja na mboga ya spinachi

Koroga hadi wiiwe kiasi

Mimina mchele, weka chumvi na maji ya moto kidogo

Funika punguza moto ili chakula kisiungue

Subiria hadi kuwiva

Andaa tayari kwa kuliwa
 

Ukipenda waweza weka mustard na fenugreek kidogo sana kwa ladha nzuri zaidi
 

Attachments

  • 1410397435133.jpg
    78.2 KB · Views: 1,646
  • 1410397515621.jpg
    100.5 KB · Views: 1,612
Thanks dada mkubwa umetisha hizi spinach hazitaiva sana kweli..
 
Hapo na samaki wa kukaanga....duh...ntakula nivimbiwe...
 

asante mama,ila siwezi kuharisha?naona kama msosi wa kigabachori huo?
 
Bibie una restaurant mahali nije kutembea na kuonja mapishi yako?


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…