Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Mara ya kwanza Dkt. Slaa akitoa maoni yake rasmi kuhusu sakata la bandari za Tanganyika kupewa waarabu wa DP world, aliweka wazi msimamo wake kuupinga mkataba ule.
Jambo la ajabu ni kuwa vyombo rasmi vya habari hapa Tanzania (hususani magazeti) yakaja na upotoshaji mkubwa huku yakitengeneza habari ya kutunga na kusema Dkt. Slaa anaunga mkono uwekezaji wa sasa wa Bandari kwenda kwa DP world.
Kilichofuata sote tunajua, Dkt. Slaa aliamua kuingia front line kuurarua vilivyo huo mkataba katika majukwaa mbali mbali ya kisiasa mpaka watawala wakaamua kumkamata na kumtengenezea kesi ya uhaini iliyokuja kubadilika na kuwa kesi ya uchochezi!
Sasa mchezo huo huo, wapambe wa watawala wameamua kuurudia tena, na sasa wametengenezea maneno ya uongo Askofu mkuu wa KKKT, Dr. Shoo eti anaunga mkono uwekezaji wa bandari zetu kwenda kwa waarabu wa DP world.
Kama mchezo huo mchafu hautadhibitiwa na watawala wenyewe, basi tusishangae KKKT kuja na waraka rasmi (utakaosomwa katika makanisa yao yote hapa Tanzania) kuhusu msimamo na maoni yao dhidi ya kuupinga na kuukosoa mkataba wa bandari na DP world ikiwa ni sehemu ya maoni yao rasmi waliyofikisha Ikulu kwa rais Samia hapo kabla.
Tuvute subira.