Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Hivi jamani... 🤔
Yanga inachangia CCM milioni 100 , halafu inarudi tena kwa wanachama wake kuwaomba michango ya uanachama.
Sasa cha kuchekesha ni kwamba hao wanachama sio wote wa CCM, wengine ni CHADEMA, CUF, ACT, UDP, TADEA, TLP… yaani kimsingi hata Mpira wa miguu una vyama vingi zaidi ya Bunge.
Ni kama kumpelekea jirani yako kilo ya sukari, halafu baada ya dakika kumi unamkuta dukani unamwomba kijiko cha sukari.
Au labda hii ni modern football politics — wanachama wanachangia chama kisichokuwa chao ili timu yao ipate sifa za “wanamapinduzi”.
Soma Pia: Klabu ya Yanga imechagia milion 100 CCM gala dinner 2025
Wengine watasema "ni mshikamano"… lakini ukiangalia vizuri, hii ni kama mashindano ya "Kutoa na Kuomba" yaliyofadhiliwa na wing ya kisiasa.
Wana Yanga bwana… Mnaweza kufunga mabao mengi, lakini mna pia record ya kufunga midomo ya wanachama wa vyama vingine kwa style ya “shida zetu ni za wote, lakini milioni zetu ni za chama fulani.”