Ni kosa kubwa sana lililofanyika, nadhani kama ingekuwa kwenye nchi nyingine ambapo mashabiki wanajielewa, wana umoja na nguvu ya pamoja ilikuwa ni kufukuza GSM na Eng Hersi wake kisha kumpa timu mwekezaji mwingine. Hapa ndipo tunaanza kuona kosa kubwa la kiufundi lililofanywa na wanachama wa Yanga ni kumpa uraisi mtu anayefungamana na upande wa GSM.Kosa walilolifanya viongozi wa Yanga kwa kuihusisha timu na ile harambee yao, litaitesa sana timu siku zijazo. Kuanzia kwenye michango ya kuichangia timu, ada za uanachama, nk.
Mdhamini naye anatoa bilioni 10 za kwenda kuwahonga wananchi masikini, halafu mpaka leo hakuna cha uwanja wa michezo walio uahidi, wala nini! Badala yake watu wanadanganywa na makombe, huku zaidi miaka 80, timu haina kiwanja chake cha mazoezi na mechi, huku timu mpya kama Azam na KMC zikimiliki viwanja vyao vizuri kabisa.