Hashpower7113
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 1,353
- 2,142
Gazeti la Mwananchi katika toleo lake la Septemba 7, ukurasa wa mbele kabisa wametumia picha ya jaji Elinaza Luvanda katika habari yao ya 'Mwelekeo Mpya Kesi ya Mbowe'.
Inafahamika kwamba picha za majaji na mahakama, huwa hazitakiwi kutumika kwenye media kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Nimewahi kuelezwa kwamba, sababu kubwa ni kwamba mahakimu na majaji, huwa wanatoa hukumu nyingi kwa watu wengi, nyingine zikiwa kali kabisa kama kunyongwa, au wakati mwingine kuwahukumu watu ambao wao huamini kama hawana hatia!
Hali hii husababisha chuki kwa watu waliowahi kuhukumiwa na jaji au hakimu fulani na kujenga roho ya visasi. Sasa unapoweka picha yake, unahatarisha maisha yake! Mawakili wasomi, hili limekaaje!