Walichokifanya Mwananchi kuweka picha ya Jaji ni sawa au ni makosa?

Hashpower7113

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,142

Gazeti la Mwananchi katika toleo lake la Septemba 7, ukurasa wa mbele kabisa wametumia picha ya jaji Elinaza Luvanda katika habari yao ya 'Mwelekeo Mpya Kesi ya Mbowe'.

Inafahamika kwamba picha za majaji na mahakama, huwa hazitakiwi kutumika kwenye media kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Nimewahi kuelezwa kwamba, sababu kubwa ni kwamba mahakimu na majaji, huwa wanatoa hukumu nyingi kwa watu wengi, nyingine zikiwa kali kabisa kama kunyongwa, au wakati mwingine kuwahukumu watu ambao wao huamini kama hawana hatia!

Hali hii husababisha chuki kwa watu waliowahi kuhukumiwa na jaji au hakimu fulani na kujenga roho ya visasi. Sasa unapoweka picha yake, unahatarisha maisha yake! Mawakili wasomi, hili limekaaje!
 
kuna wengine siyo majaji ni vibaka tu waliovamia mahakama zetu, Jaji anayejielewa hawezi kukubali kutumika na chama cha siasa
 
Kama jaji au hakimu anafanya mambo kipumbavu pumbavu kwa kufuata maagizo ya hovyo hovyo anastahili kushughulikiwa accordingly n perpendicularly
 
nimesoma content yake na yako, wote hamjaainisha huo utaratibu.

wekeni hapa hicho kifungu kinacholeta huo utaratibu.
Kwa hiyo wewe hoja yako hapo ni kwamba unajua hakuna utaratibu unaozuia majaji kuwekwa picha zao kwenye gazeti au unajua upo ila unaona si vyema kuwa na utaratibu kama huo kwa kuwa nao ni binadamu kama wengine? Tuanzie hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…