Walichopata madaktari baada ya mgomo

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Kijana daktari anayetokea chuo bila ujuzi (medical intern) atakua anapiga mpunga wa kitita cha Kshs 196,244 (Tshs 4,513,612)

Daktari Kenya anayeanza taaluma, yaani entry level ya job group N (mid-level medical officer) mshahara wake umepanda kutoka Ksh 146,190 (Tshs 3,362,370) hadi Kshs 241,524 (Tshs 5,555,052) hii ni pamoja na mafao mengine saba.
Wale specialist mishahara yao imepanda hadi Kshs 442,060 (Tshs 10,167,380) pamoja na mafao lukuki.

Hongera zao, ila ingekua bora maafikiano kama haya yanatekelezwa bila maafa kwa Wakenya, wengi tumeteseka kisa pande zote mbili hakuna aliyekua tayari kushuka. Natumai na kuomba wana taaluma zingine wasiingie kwenye migomo na pawe na jinsi ya kuwarekebishia maana tukiendelea hivi, sitashangaa kuwaona wanajeshi wetu nao wamegoma japo hawaruhusiwi.


Death, pain: Cost of hospital strikes
 
Acha ungo hakuna mafikiano yaliopatikana Kenya serkali imekataa kuzungumza Na madactari had I warudi Kwanzaa kazini
 
Hao wamepata chapaa poa, expect migomo wa madaktari kwa majirani sasa kwa vile watakuwa wanaji compare na wenzao

Sio kwa enzi ya Magufuli, tena yule hawawezi kumjaribu maana alishasema asijaribiwe. Wathubutu kugoma goma huko Tanzania ndio watajua pushups alizokua anafanya wakati wa kampeni zilikua na umuhimu fulani.
 
Sio kwa enzi ya Magufuli, tena yule hawawezi kumjaribu maana alishasema asijaribiwe. Wathubutu kugoma goma huko Tanzania ndio watajua pushups alizokua anafanya wakati wa kampeni zilikua na umuhimu fulani.
Hahahahahaha mkuu umeifanya asubuh yangu iwe nzur nimecheka mpaka tumbo limeniuma jaman afu saiv ukigoma kuna vijana weng hawana ajira kwahy ukigoma anatangaza ajira watu wakakureplace
 
Baba goes out of the country and all the strikes are resolved, isorait
 


Kenya wana Uchumi mkubwa hivyo wanaweza labda kulipa, lkn pia wasiwasahau wengine wanaokufa njaa kwa kukosa hela ya chakula kwa kuwa tu hawana lobby wa kuwapigania mpaka wakumbukwe na donors ktk nje!
Halafu vp kuhusu Wauguzi (nurses) Mishahara yao imepanda kwa kiasi gani kwa maana umeonyesha ya Madakrari tu ningependa kujua pia!
 
Sasa wanapata kile kinachoendana na elimu yao,uku kwetu huo mgomo ukitokea watanyongwa hadharani.
 
Hongereni wa Kenya. Mwisho wa siku hakuna aliyetolewa kucha. Kila la heri mnaposogea hatua kwenye uchumi wa kati.

Watanzania tujifunze. Nchi haiwezi kuendelea kama wanaoneemeka ni wanasiasa tu.
 
Huu ndo umuhimu wa watu kusimama pamoja na kutetea maslahi yao. Kuna madungayembe nchi nyingine yana phd na professional qualifications zote kutwa kujipendekeza kwa wanasiasa na kuendekeza njaaa.
Kuna mmoja ni waziri Wa sheria sijui..jamaa mnafiki dunia nzima!
 
Kenyan intelligence community ni dhaifu mno,soon mtasikia madaktari wanagoma tena sababu hiyo danganya toto yao haiwezekaniki ghafla hivyo.
 

Ujue halafu iweje....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…