Walikuja kwa sura ya dili la biasharakumbe matapeli,kaa chonjo!!!!!

10Shoka14

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
305
Reaction score
122
Wanajamvi namshukuru Mungu wangu aliyehai ninayemuabudu kwa kuninusuru na utapeli uliokuwa ukisukwa juu yangu.

Hatari sana,ni kitu ya mchana huu.Kanipigia mtu kupokea kanisalimia kwa kunichangamkia sanaaaa,mpaka nikaona hii sasa noma kumuuliza nani sijui atajisikiaje.Nikamvutia kasi baada ya salamu za utangulizi nikamwambia hapa kwetu tunashukuru neema ya mvua imekuja vipi huko?

Huku sisi bado,sawa samahani naomba usijisikie vibaya nani naongea naye aaaah inamaana umepoteza namba yangu?Nikapigwa swali,jibu umepatia ndo maana nakuuliza Mi j4 ahaa shemu,ndiyo za ---?Nzuri lakini siko hapo kwa sasa niko Arusha nimepata kibarua hapa AICC mi ni dereva.

Ok hongera,nashukuru akajibu.

Sasa shemu hapa nilipo kunaboss wangu kanipa tender ye anafanyia UN.Kuna watu kutoka Sudan ya kusini huwa wananunua dawa za Kuhifadhia nafaka.

Huwa wanafanya na mdogoake huyu boss wangu ninayemuendesha ila kwa sasa yupo uganda masomoni,na hawa wageni wameshafika ila wanahitaji mtu wa kusupply hizo dawa. Gidion Lima alikuwa ndo anafanya hii kazi sasa niliulizwa na Boss kama nina mtu mwaminifu ninayemfahamu nikaona utanifaa na hauta niangusha.
Uko sasahihi,kwahiyo nini unachotaka nikifanye kwa kuvaa viatu vya Gidion aliyeko masomoni?

Kuna namba za agent wa UN yuko hapo mkoa wa.....ndo huwa anauza hizi dawa.We mpigie mueleze ni mdogo ake Gidion,then muulize kama dawa zipo,bei ya dawa kwa pair inakwendaje kwa sasa,na kama zipo tunaweza pata pair mia tatu leo(300)?

Halafu nipe jibu niulize mkalimani wa wale wageni wananunua kwa kiasi gani ili kuona kama kutakuwa na faida tufanye nao kazi.Poa Nashukuru utaratibu wa kusajili namba,nikahitaji kufahamu jina la J4 nikakuta ni Benjamini Willium no.0769721953 (shemeji bandia).

Nikaona ngoja niende kwa agent J4 aliniambia anaitwa Mzee Dickson lkn jina alilosajili ni Yohana Paulo no. 0754695542 nikampigia simu ikaita mpaka ikakatika hakupokea.

Mara akapiga samahani nilikuwa nahudumia wateja sikuweza kupokea simu yako,haina shida mzee Dickson.Nikafanya kama J4 alivyonielekeza nikapata jibu dawa zipo,bei ni Tsh. 50,000/= kwa pair.Nikauliza je ktk stock yako tunaweza pata pair 300 nikajibiwa naam na zaidi ukihitaji.

Wakati namaliza mazungumzo na Dickson nikachukua karatasi nililokuwa nimeandika namba zao majina bandia na majina halisi halafu nikaona bado sijajua ni kitu halisi au matapeli.

Nikampigia Dada yangu mara mbili hakupokea.Nikapata namba ya shemeji halisi nikakuta ni tofauti na ya bandia j4 nikafikiri halafu nikajisemea kimoyo moyo isiwe tabu labda ananamba mbili. Kucheki jina kwenye M-pesa jina la kwanza naye ni Willlium lapili tofauti na la J4.

Akili ikanicheza nikarudi kwa Dada jina lake la pili linamatch na la Shemeji halisi.Nikasema sasa natumia fani yangu kidogo ya Dr na Cr.Alipiga na namba mpya Mimi nampigia kwenye ile ya zamani ili kuitendea haki Golden rule in Accounts.

Akapokea shemeji halisi baada ya salamu nikamuuliza habari ya wapi akanieleza ya ....ambapo ndo makazi yake yalipo.Kunamtu nilimuona Arusha ni wewe au nilifananisha?Hapana Shemeji mi sijawahi hata kufika Arusha,basi nakushukuru tukaagana.

Mara J4 akaja hewani,ehh vipi ushaongea na mzee dickson ndiyo sa mbona hujanipa jibu Shem nikamwambia ndo nimemaliza mazungumzo sasa hivi.

Nikampa mrejesho akaniambia sasa mpigie mkaliman ili ujue wao watanunua kiasi gani?Ili kama inalipa tufanye kazi unapeni hapo nikutajie namba,ndiyo no. yake ni 0755201695 anaitwa Gloria.Nikamwambia mi nawazo tofauti kwa kuwa mi nimecheki na mzee Dickson we ungecheki na Gloria halafu utanipa jibu,aahhh shemeji sasa we hauko serious kama hauko tayari basi ngoja nimtafute mtu mwingine nikamwambia sawa.
Kwenda kwenye M-pesa Gloria jina ni Gloria Kagari.

Basi ndo movie ilivyokuwa hivyo namshukuru Mungu tena kwa kuninusuru na matapeli walio wavivu wa kutafuta ngawira kwa njia zilizo halali.USHAURI WANGU TUJITAHIDI KUPASHANA HABARI ZA HAWA WENYE MBINU CHAFU ZA KUTAKA KUKWAPUA FEDHA ZETU ISIVYO HALALI,NAWASILISHA.
 
Huu mbona utapeli wa kizamani, wengi walishalizwa na hawa jamaa.
 
Wewe umechemka kweli.
Kwanini usiweke mtego na Polisi.
Yaani unaishi Dar unakuwa Mshamba kiasi hiki?yaani umeniboa kweli,likuwa haina hata haja ya kuweka uzi huu hapa.
Bora wangekutapeli ndio akili ya kuishi mjini ingekuja.

Ngoja nikupe mtego wa watu kama hao.
Wewe ungetoa taarifa kituo cha polisi mapema sana.Then Polisi wangewasiliana na Kampuni ya Sima kisha hizo sim wangeziangalia zinatumia minara ya Mkoa gani,wilaya gani na eneo Gani.
Maana Kampuni za Simu zinauwezo wa kujua mtu anetumia sim hii yupo wapi na Mnara anaotumia ni wawapi na number ya mnara ni ipi.
Then ungewekwa Mtego mmoja Mtam sana na mtandao wote ungekamatwa.
Maana jinsi kampuni za sim zilivyo na hasira na watu hao na polis walivyo makini kipindi hiki,Mbona wangemjua Kova ni nani.
 
10Shoka14 wewe unaishi wapi kaka, mbona utapeli wa miaka mitatu iliyopita?...yaani hata huyo tapeli mwenyewe nadhani anajifunza, wenzake walishatapeli kitambo sana wakaacha!
 
Last edited by a moderator:
Wiki 3 iliyopita walijaribu kwangu, nikawaambia wanitur 500,000 kama kianzio na baada ya kufuatilia nikagundua wako jirani na ppf tower
 

amefanya jambo la maana sana kuachana nao kuliko kwenda polisi,tanzania hii kwa sasa haina mwenyewe na hali ya ulinzi ni dhaifu sana hasa kwa raia mmoja mmoja(hasa kwetu sisi wa hali ya chini)na mbaya zaidi intelijensia ya nchi hii iko kaburini.unaweza ukawakamatisha kumbe wana mitandao,manake mahakamani ni lazima wewe ndo shahidi namba moja,matokea yake wakakuwinda ukamwagiwa mitindikali bure,au ukala kitu cha ufoo saro.hapo hakuna cha polisi wala cha kiongozi yeyote atakaye kusaidia eti kwa kuwa ulionyesha uzalendo.kwa sasa hali ilivyo,kama mtu anakupa dili na hautaki,ni bora umwambie hautaki na ukae kimya,ukijitia kimbelembele cha kukamatisha matokeo yake wata kuhome shopping center ubaki unajifia mwenyewe.na huwezi jua kama hata hao police huwa wanashirikiana
 
hao matapeli waliwahi kuwekewa mtego na ferald hando wa clouds fm waliaibikaje on air!!
 
Huu mbona utapeli wa kizamani, wengi walishalizwa na hawa jamaa.

Lengo langu halikuwa kupost utapeli wa kisasa.Makusudi ni kuwatahadharisha ndg zangu ambao hawajafikiwa ili watakapofikiwa waweze kosoma mchezo unaoendelea.
 

Nina marafiki kibao mapoti ambao ningetaka tufanye nao kazi ningeamua niwaombe wangapi kwa idadi wanisaidie,lakini nilifanya mahesabu nikaona yanakataa,hasa hasa swala la muda.

Fikiri kama ningemnasa labda mmoja tu kwa maana kama Dickson piga ua garagaza ilikuwa lazima nikutane naye uso kwa macho.

Labda wangampiga ndani halafu akatakiwa kufikishwa mahakaman huoni ningeacha shughuli zangu za kuwajibika kwa ajili ya Mungu wangu,Familia yangu na Taifa langu,nilipofikiri haya nilighairi kufanya lolote nikaona niachane nao kiroho safi.
 
10Shoka14 wewe unaishi wapi kaka, mbona utapeli wa miaka mitatu iliyopita?...yaani hata huyo tapeli mwenyewe nadhani anajifunza, wenzake walishatapeli kitambo sana wakaacha!

Mimi mtu wa kuamsha amsha mwanzo mwisho.
Siunajua kutafuta shilingi!
Nakuwa safari muda mwingi ndani ya Tz.
 
Wiki 3 iliyopita walijaribu kwangu, nikawaambia wanitur 500,000 kama kianzio na baada ya kufuatilia nikagundua wako jirani na ppf tower

Basi kama ni ndani ya wiki tatu inamaana aliyesema ni mtindo wa miaka mitatu iliyopita atakuwa anaelewa sasa,kwamba wamerudi tena hawa matapeli.
 

Mkuu kozo we unaona mbali,unauwezo wa kupima mambo kwa upana wake.
Nafikiri walionilaumu kwamba nilikosea wanapopita kwenye post yako wanapata kuelewa kwann niliachana nao bila mikwara.
 
hao matapeli waliwahi kuwekewa mtego na ferald hando wa clouds fm waliaibikaje on air!!

Mbona mwandiko wako kama wa yule mkali......
Nakutania sis. tunakushukuru kwa kuchangia
 
Mkuu kozo we unaona mbali,unauwezo wa kupima mambo kwa upana wake.
Nafikiri walionilaumu kwamba nilikosea wanapopita kwenye post yako wanapata kuelewa kwann niliachana nao bila mikwara.

hiyo ndo hali halisi wangu,tanzania sio ile ambayo tunaifikiria akilini mwetu
 
"MKUU WETU WA NCHI ALISEMA" ukitaka kula na wewe kubali kuliwa.
 
umenifungua macho bestito ila utapeli huu ni wakkizamani sana
watu kila leo wanalizwa na hawa jamaa kwanini hamkutumia mabenki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…