Walimu 13 wafukuzwa kazi Bagamoyo sababu ya utoro

Walimu 13 wafukuzwa kazi Bagamoyo sababu ya utoro

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Walimu 13 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wamefukuzwa kazi kutokana na makosa ya utoro huku wengine wanne wakiendelea kujadiliwa kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo kujihusisha na mapenzi na wanafunzi pamoja na ulevi uliopindukia katika kipindi cha miaka miwili kuanzia 2020 hadi Septemba

Katibu wa tume ya utumishi wilayani humo Fedinand Ndomba amesema tabia ya utoro inayofanywa na baadhi ya walimu imekua ikichangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hivyo uamuzi wa kuwafuta kazi walimu hao ni ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wenye tabia kama hizo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa wa Pwani Douglas Mhini ameeleza changamoto zinazowakabili walimu ikiwemo kucheleweshwa kwa fedha za uhamisho pamoja na malipo kwa wastaafu.

Naye katibu tawala wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni akimuwakilisha mkuu wa wilaya amekemea vitendo viovu vinavyofanywa na walimu na kamwe hatovifumbia macho vitendo hivyo

Chanzo: EATV
 
Dhuluma ya haki mbalimbali mfano, mshahara usioendana na uhalisia wa ghalama za maisha, malimbikizo ya mshahara, kutopanda madaraja kwa wakati, kukosa motisha na upendeleo ktk kutoa motisha na mengine mengi wanazofanyiwa walimu zinapelekea wanafrastrate hadi ulevi kupindukia kutokana na kukata tamaa ya maisha!
 
Halafu ukute walikua wanatoroka kwenda kula bata, ila kama walikua wanatoroka kwenda kwenye mishe nyingine za kuwapatia chapaa sio mbaya
 
Usipoheshimu kazi, lazima utakutana na kadhia tu kama hizi
 
Dhuluma ya haki mbalimbali mfano, mshahara usioendana na uhalisia wa ghalama za maisha, malimbikizo ya mshahara, kutopanda madaraja kwa wakati, kukosa motisha na upendeleo ktk kutoa motisha na mengine mengi wanazofanyiwa walimu zinapelekea wanafrastrate hadi ulevi kupindukia kutokana na kukata tamaa ya maisha!
Na ahadi Hewa za CCM
 
Hao watoro lazima hawakuonekana mwaka mzima, tena walipoitwa wakawa hawajaja au wakawa wajuaji.

Ukifukuzwa ualimu umeyaanzisha mwenyewe.
 
Hongereni walimu wote mliofukuzwa kazi. Utulivu tu ndiyo kila kitu katika maisha yenu mapya ya kitaa.

Wakati fulani kuajiriwa katika kazi yenye changamoto nyingi na inayo dharauliwa mpaka na ma failure kibao tu wa form four kama ya ualimu, ni ujinga tu.

Mtaani fursa ni nyingi sana kama una mtaji.
 
Yaani watakuja kuwashukuru waliowafukuza kazi
 
Ujinga mtupu wengine mnaotudharau walimu hate hamna take home ya 1000k...
 
Back
Top Bottom