Walimu 6 walioonekana katika video ya watoto wakiigiza ngono wafikishwa Mahakamani

Walimu 6 walioonekana katika video ya watoto wakiigiza ngono wafikishwa Mahakamani

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Walimu sita wa Kenya wamefikishwa mahakamani, baada ya kukamatwa kwa video ambayo walionekana kuwaruhusu watoto wa shule ya msingi kuiga vitendo vya ngono, katika shule moja magharibi mwa nchi.

Video hiyo ilisambazwa sana nchini Kenya na kusababisha hisia kubwa ya umma.

Walimu hao walikamatwa baada ya maafisa kutoka Wizara ya Elimu kuanzisha uchunguzi kwa mujibu wa Osob Elmi kutoka Nairobi.

Katika sekunde 29 za kipande hicho cha video, ambacho kimesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, wavulana wanne waliovalia sare wanaombwa na walimu wao kulala juu ya kila mmoja huku vicheko vya watu wazima wanaodhaniwa kuwa walimu vikisikika kwa nyuma. Mmoja wa watoto baadaye anaonekana akilia.

Waziri wa Elimu wa Kenya ametoa wito wa kufutwa kazi na kuchukuliwa hatua za kinidhamu walimu hao sita wanaofanya kazi katika shule moja Magharibi mwa Kenya.

Wakati wa kukamatwa polisi walithibitisha kuwa video hiyo ilichukuliwa shuleni.

Jaji sasa ataamua ni mashtaka gani yatachukuliwa dhidi ya walimu hao.

 
Back
Top Bottom