KERO Walimu ajira mpya 2026 Babati tunachelewa kwa fedha za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaomba msaada wa kutupazia sauti sisi watumishi wa ajira mpya wa mwaka 2026 katika Idara ya Elimu, Halmashauri ya Babati.

Hadi leo imepita takribani miezi saba tangu kuajiriwa kwetu, lakini bado hatujapokea fedha za kujikimu ambazo ni stahiki yetu kwa mujibu wa taratibu za utumishi.

Kuchelewa kwa malipo haya kumetuletea changamoto kubwa, hasa kwa wale tuliopangiwa vituo vya kazi mbali na maeneo yetu ya awali ya makazi.

Tunaomba mamlaka husika zitusaidie kutoa ufafanuzi na kuhakikisha suala hili linapatiwa ufumbuzi kwa wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…