KERO Walimu AJIRA mpya halmashauri ya wilaya ya Nzega -Tabora hatujalipwa pesa ya kujikimu

KERO Walimu AJIRA mpya halmashauri ya wilaya ya Nzega -Tabora hatujalipwa pesa ya kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

TOSHI 124

New Member
Joined
Jun 21, 2026
Posts
1
Reaction score
0
Halmashauri ya wilaya ya Nzega -Tabora haijatulipa fedha za kujikimu walimu wa ajira mpya 2026 badala yake imewalipa watumishi wa afya pekee, hii sio haki kwa watumishi wengine Kwani wote tuna haki ya kulipwa fedha hizo, mkurugenzi amekaa kimya na hakuna majibu ya kueleweka kuhusu jambo hili.
 
Kada yenu imedharaulika sana nyakati hizi kwa kujifungamanisha na CCM, wezi wa Mali ya Umma na Kura za CHADEMA..hakuna atakaye kujali hapa JF ...Labda - Mwashambwa na Tlaatlaah-ambao nao ujira wao ni elfu 7 tu kila wakiandika kuitukana CHADEMA / Heche,hapa JF na ni ndogo haiwatoshi hata wao..

Hiyo hela imetunzwa kwa ajili ya kumchukulia Fomu Mgombea wa Uraisi-CCM-2030.

Bashe ana Mwashamba hapo Nzega..kafanyeni vibarua kwake muweze kuishi.
CCM hawana habari na nyie maana chaguzi bado mbali.
 
Walimu n CCM lenu ni moja.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Sisi kutoka Nzega - Tabora kero yangu naomba muipaishe ni juu ya sisi Walimu ajira mpya wa Mwaka 2026 tangu January 2026 hadi sasa bado hatujapata fedha za kujikimu na hii ni Nzega Vijijini tu wenzetu wa Nzega Mjini walishapewa muda ila sisi mpaka saizi bado.
 
Back
Top Bottom