KERO Walimu ajira mpya Januari 2026 tunaendelea kulalamikia kutopewa fedha za kujikimu

KERO Walimu ajira mpya Januari 2026 tunaendelea kulalamikia kutopewa fedha za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi ni walimu wa ajira mpya tulioajiriwa mwezi Januari 2026. Kwa muda sasa tumekuwa tukifuatilia malipo ya fedha zetu za kujikimu, lakini hadi sasa hatujapata majibu yoyote rasmi kutoka kwa mamlaka husika.

Tumeingia mwaka mwingine wa fedha bila kupata ufafanuzi kuhusu hatima ya stahiki hizi, hali ambayo inakatisha tamaa na kutuongezea changamoto katika utekelezaji wa majukumu yetu.

Tungependa kupata kauli rasmi, hata kama ni kutueleza kuwa walimu hawastahili malipo hayo, ili tujue msimamo wa mamlaka husika. Hii ni kwa sababu tumeshuhudia baadhi ya watumishi wapya katika sekta ya afya wakilipwa stahiki hizo, huku sisi walimu tukiendelea kusubiri bila taarifa yoyote.

Tunaomba JamiiForums itusaidie kufikisha kilio chetu ili sauti zetu zisikike. Kukosa fedha hizi za kujikimu kumetuweka katika mazingira magumu, hasa kwa walimu wengi waliopangiwa vituo vya kazi mbali na maeneo yao ya awali ya makazi.

Tunaomba mamlaka husika itoe ufafanuzi na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma.
 
Back
Top Bottom