Walimu ajira mpya ogopeni CWT mtalia kama tunavyo lia sisi

Walimu ajira mpya ogopeni CWT mtalia kama tunavyo lia sisi

Qualifier

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2012
Posts
1,252
Reaction score
405
CWT, ilianzishwa kwa nia njema ya kutetea na kudai maslahi ya walimu, lakini sasa viongozi wamesha poteza dira wamegeuza CWT kuwa chama cha kuwanyonya walimu na kutumia jasho la walimu kujengea majumba makubwa, kujilipa mishahara minono kufanya mashindano ya kununua magari ya kifahari huku wameacha walimu wanao dai madeni toka serikalini kila mtu adai kivyake kama vile hakuna chama cha walimu. Walimu hawajalipwa madeni yao sasa ni muda mrefu na CWT wamekaa kimya kama vile hakuna walimu wanao idai serikali ninawashauri walimu mnao anza ajira msijaze form za CWT hawana mpango na walimu tena vinginevyo walimu wasingedai serikali kwa muda mrefu kiasi hiki na CWT wako kimya
 
point.....
wasipouchukua ushauri huu hakuna ushauri wa maana watakaokuja kuuchukua
 
Iyo fomu ata kuiona sitaki,ntachapa mtu kibao
 
Ok asante mkuu,ila nimesoma nyaraka moja wapo inasema mwalimu halazimishwi kujiunga ila kwa wale ambao c wanachama wanalazimika kukatwa asilimia mbili ya mishahara yao hii inamaana uwe ama usiwe mwanachama hela yako lazima iliwe na cwt(huu ni unyonyaji kabsaaa ) sasa cjajua kwawalewanachama huwa wanakatwa asilimia ngap? Binafsi siipendi cwt!!
 
Mi sitaki hata kuisikia.cwt ni kichefuchefu,ni wakati sasa kuwe na vyama vingi vya walimu.
 
Kumbuka Umoja ni Nguvu ipo siku utaiona CWT ya maana.Tatizo kubwa serikali ya ccm imefilisika.WITO KWA WAALIMU POPOTE MLIPO ENEZENI ELIMU YA URAIA KWA WAZAZI WAIKATAE CCM
 
walimu wote wanakatwa asilimia 2,uwe umejiunga au la! Mungu saidia hili taifa la Tanganyika.
 
Wapendwa, wanaoidai Serikali siyo walimu pekee. Hata wajasiriamali tunaidai serikali. Serikali imefilisika mtachefuana bure na kutukanana bure.

Wanachama wanakatwa 2% na wasiowanachama ni hiyo hiyo 2%. Kwa taarifa yako ni bora uwe mwanachama kwa vile kuna mengi mazuri yanakuja. Kujenga majengo ni suala muhimu japo yaliyopo sasa yanatosha na jitihada zinafanywa kuona namna mwalimu anavyoweza kunufaika na makato anayochangia CWT. Japo si mwalimu, sikushauri usijiunge kwani hauna cha kupoteza ukijiunga sana sana kwa mwelekeo uliopo sasa watakaojiunga na CWT watanufaika zaidi siku za usoni.
 
CWT inamanufaa unapopata tatizo,kama huna tatizo haina manufaa.Mkurungezi wa CWT akiwa DUCE Kwa ajili ya ufunguzi wa tawi la UDSTA,amedai kuwa CWT imesaidia waalimu wengi sana ktk kesi zilizokuwa zikiwakabili,pia imewasaidia waalimu wanawake hususani wanapopata ujauzito,imesaidia kudai nyongeza ya mishahara ya waalimu na mengine bado yanatekelezwa na serikali.
Kwa hiyo fikiri kabla ya kutenda kujiunga au kutojiunga na CWT,pia walisema kuwa uwe au usiwe mwanachama kukatwa 2% ni palepale.
 
Ok asante mkuu,ila nimesoma nyaraka moja wapo inasema mwalimu halazimishwi kujiunga ila kwa wale ambao c wanachama wanalazimika kukatwa asilimia mbili ya mishahara yao hii inamaana uwe ama usiwe mwanachama hela yako lazima iliwe na cwt(huu ni unyonyaji kabsaaa ) sasa cjajua kwawalewanachama huwa wanakatwa asilimia ngap? Binafsi siipendi cwt!!
Ni sheria ya kazi, kama kwa mwajiri asilimia 50 ni wanachama wa trade union, wengine wote mnakuwa wanachama pia, wakitaka waanguke na hiyo sheria!
 
Sio CWT vyama vyote havifai, kwanini iwe lazima kuwa mwanachama? Ila ujinga huu ulianzia mavyuoni kwenye serikari za wanafunzi mara utasikia DARUSO, DITSO..... Huku ndiko ujinga unaanzia kisha tunakuja kwenye TUICO, TRAU, TUGHE..... Full wizi na semina za kumwaga. Thanks god sina chama chochote kuanzia kwenye mipira, siasa wala vyama vya kazi
 
Ok asante mkuu,ila nimesoma nyaraka moja wapo inasema mwalimu halazimishwi kujiunga ila kwa wale ambao c wanachama wanalazimika kukatwa asilimia mbili ya mishahara yao hii inamaana uwe ama usiwe mwanachama hela yako lazima iliwe na cwt(huu ni unyonyaji kabsaaa ) sasa cjajua kwawalewanachama huwa wanakatwa asilimia ngap? Binafsi siipendi cwt!!

haya maneno hata mie nimeyasikia huko niliporipoti!
 
Back
Top Bottom