balimar
JF-Expert Member
- Sep 18, 2015
- 7,743
- 13,657
Wadau Habari!!
Leo tulikuwa na kikao cha Maafisa Elimu Kata na Walimu wakuu kujadili Mambo mbalimbali ya kuboresha taaluma wilayani kwetu
Mwenyekiti wa CWT wilaya alipopewa nafasi ya kuongea alielezea swala la Bodi ya Kitaalamu ya walimu na sintofahamu ya Makato. Kitu kilichosikitisha ni yale ambayo Bodi hii mpya inataka kufanya kwa Walimu. Kiukweli serikali itusikie sisi walimu makato yanatosha jamani.
Uwelewa duni wa walimu kuhusu bodi (TPB) ndio mtaji wa wapigania Bodi. Teacher Profesional board sio trade union (cwt) na wala sio substitute ya trade union maana tunalo kato la kisheria na kanuni za CWT sasa inakuja Board ya Walimu ikiwa imebeba mitihani ya kila mwaka kwa mwalimu na malipo ya Leseni ambazo tozo zote zinataka mshahara duni wa mwalimu. Lakini hii bodi majukumu yake yanayoainishwa yapo na yanatekelezwa na TSC ambayo hatulipi chochote wala hatufanyi mitihani chechefu.
Lakini hilo likishindikana maana yake, Sheria ya TSC na kanuni zake zikapita zitatumika zote. Cwt kama Trade Union kwa sheria na kanuni zake, TSC na mambo yake na mwisho ni TPB na sheria zake na mitihani na ada na leseni zake za kila mwaka ambao ndio zigo lenyewe kwa Mwalimu ambapo Cwt wanahimiza wanachama waikatae kwa kutoa maoni yao kwani haina tija.
Serikali tunaomba hiyo Bodi bakini nayo sisi walimu tuboresheeni TSC makato ni mengi mshahara wenyewe njiwa huu
Nawasilisha