Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imeandaa mikakati kwa kila mwalimu wa shule ya sekondari kuvaa sare ya suti kwa ajili ya matukio mbalimbali.
Mkuu wa mkoa huo, Albert Chalamila amesema wameandaa baadhi ya sare za walimu zitakazotumika katika mikutano mbalimbali.
Amesema baada ya kukabidhiwa kitambaa cha suti, kila mwalimu atapewa shilingi elfu 80 taslimu.
"Shilingi elfu 50 itakuwa kwa ajili ya kiatu na elfu 30 kwa ajili ya mashono," amesema Chalamila