Walimu ivuna sec wamegoma kuingia madarani

mwela

Member
Joined
Apr 26, 2011
Posts
47
Reaction score
7
Hatimaye walimu wote wa shule
ya sekondari lvuna ilioko kata ya
lvuna tarafa ya kamsamba wilaya
mpya ya MOMBA wamegoma
kuingia madarasani kuanzia leo tar
18.03.13 mpaka watakapo
tekelezewa madai yao sugu.
Madai hayo ni ukosefu wa
nyumba za kuishi ambapo tangu
shule hiyo ianzishwe mwaka 2007
hakuna nyumba iliyo kamilika japo
walimu hao wamekua wakiishi
kwenye magofu hayo.ambapo
gofu moja wanaishi walimu
watatu watatu kwa kila gofu jambo ambalo
husababisha adha kubwa kwa
walimu hao.
Aidha walimu wa kike
wamelazimika kuishi pamoja na
wanafunzi ktk jengo la Hostel.
Walimu hao wamelazimika kugoma mara baada ya kutelekezwa na uongozi wa kata hiyo kwa kukaidi wito.
 
Ni vyema serikali ikachukua hatua za haraka juu ya malalamiko ya walimu hao,la sivyo ili tatizo la division0 litabaki kuwa sugu
 

Madarani=madarasani?
 
Kwa shule za Kata, serikali ilikurupuka, japo kuwa mwasisi wake, Waziri Mkuu aliyeiuzulu, Mh. Edward Lowasa hapendi kusikia hivyo.
Kwa bahati mbaya zaidi, kabla ya shule hizo nyingi kama utitiri kutengamaa, mwasisi wake akaondoka madarakani kwa shutuma za rushwa. Alipoingia Waziri Mkuu mwingine (wanayemwita mtoto wa mkulima), Mh. Mizengo Pinda akapandisha sera ya Kilimo Kwanza. Jambo lilofanya shule za Kata kuwa taabani.
Huku Kilimo Kwanza, kama ilivyo kwa shule za Kata, kuonyesha dalili zote za kushindwa, muda unakwenda na rasilimali zinaangamia kwa hasra. Naamini Raisi amekuwa msikivu sana, hata kujikuta akikubali mawazo kama haya, au sijui na yeye alishauriwa vibaya.
Mwishoni mwa mwaka 2015 kutakuwa na W. Mkuu, pamoja na serikali nyingine, sijui kipaumbele kitakuwa nini? Wachambuzi wakisema "Tanzania ni kama kichwa cha mwendawazimu" wanaambiwa siyo wazalendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…