KERO Walimu katika halmashauri ya Mbozi hatupewi nafasi ya kuchagua chama cha wafanyakazi tunachotaka, tunalazimishiwa CWT

KERO Walimu katika halmashauri ya Mbozi hatupewi nafasi ya kuchagua chama cha wafanyakazi tunachotaka, tunalazimishiwa CWT

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaomba kufikishwa kwa mamlaka husika malalamiko yetu kutoka kwa walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kuhusu changamoto inayojitokeza katika suala la uchaguzi wa vyama vya wafanyakazi.

Kumekuwa na malalamiko kwamba watumishi wa kada ya ualimu wanazuiwa au kushinikizwa kubadilisha au kuchagua vyama vingine vya wafanyakazi, na badala yake kulazimishwa kubaki katika chama cha wafanyakazi cha CWT.

Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa haki za msingi za mfanyakazi, mtumishi ana uhuru wa kuchagua chama cha wafanyakazi anachotaka kujiunga nacho kati ya vyama vilivyosajiliwa na vinavyotambulika kisheria. Hivyo, kuwepo kwa madai ya kulazimishwa kubaki katika chama kimoja kunazua maswali kuhusu uhalali na ufuatiliaji wa haki za watumishi.

Changamoto kubwa inayoulizwa na walimu ni kwa nini wanazuiwa kuchagua vyama vingine vya wafanyakazi ilhali sheria na taratibu za kazi zinatoa nafasi ya uhuru wa kuchagua uanachama.

Kutokana na hali hii, tunaomba mamlaka husika ifuatilie kwa karibu suala hili ili kuhakikisha kuwa haki za watumishi zinalindwa, na kila mfanyakazi anapewa uhuru wa kuchagua chama cha wafanyakazi anachokipenda bila shinikizo au kulazimishwa.

Tunasisitiza kuwa uwazi, huru na haki katika uanachama wa vyama vya wafanyakazi ni msingi muhimu wa ustawi wa watumishi na ufanisi katika utendaji kazi.
 
Back
Top Bottom