Walimu Makada wa CCM wamempatia Tuzo ya utendaji uliotukuka Mbunge Aeshi Hilaly

Walimu Makada wa CCM wamempatia Tuzo ya utendaji uliotukuka Mbunge Aeshi Hilaly

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly amekabidhiwa tuzo ya utendaji uliotukuka na kuendeleza michezo, tuzo ambazo zimeandaliwa na Walimu Makada wa CCM Manispaa ya Sumbawanga.

Mbunge Aeshi amepokea tuzo hizo alizokabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Silafu Maufi ikiwa ni kutambua mchango wake kimaendeleo Katika Mkoa wa Rukwa ukitambulika kama utendaji uliotukuka na juhudi za kusaidia vijana kimichezo kupitia Michuano ya @aeshsuper_cup

Tuzo hizo amekabidhiwa katikati ya Juma hili katika Ukumbi wa Mikutano wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa.​

chanzo:Vosfmtz​
 
Aeshi elimu yake ya kawaida tu,nasikiaga aliishiaga kidato cha pili,ila yuko very smart kwenye mienendo yake kisiasa.Anakubalika sana pale S'wax,anasemwa ni mtu wa watu.Bilasgaka kwa analysis ya kawaida,yeye(Aeshi) ni mbunge anayeongoza kwa kukubalika kule Rukwa,anafuatia Kenani wa Nkansi,then Deus Sangu(aliyetengenewa zengwe majuzi),ĥalafu Vincent Mbogo anafuatia wa mwisho ni Kandege ambaye asipoangalia anaweza akadondoshwa safari hii kama ana azma ya kugombea tena,Steven Sakalani angemuondoa kirahisi endapo CHADEMA wangemsimamisha ashindane na Kandege.Kila la heri Aeshi.
 
Back
Top Bottom