walimu na kauli zao!!!!!

walimu na kauli zao!!!!!

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643
salamu wakubwa!!!

aiseee,, walimu ni walezi wetu kwa upande mmoja ama mwingine, lakini wakati mwingine wanaboa kwa kauli zao!

hebu tujikumbushe kidogo kauli za walimu wetu (ziwe njema ama mbaya!)

1.hata nikeshe nafundisha, wengine hawatoki na lolote!!

2. hata msipoelewa, mshahara wangu uko pale pale!!

3. bichwa lako kubwa lio kwa ajili ya kutenganisha masikio yako!!

4. wengine hapa wapo kwa ajili ya kukua!

5. ulivyo wewe ndivyo kulivyo kwenu! (naona kama kuna ukweli ndani yake!!!!)

6. ulikuja peke yako, utaondoka peke yako! ( maarufu sana wakati wa sp)..

....... ongezea kali nyingine!!
 
Mtaala unaelekeza tuwape 25%.! Hizo 75% Mtajitafutia wenyewe
 
Ukipika maharage kuna mengine machache huwa hayaivi.
 
"Wengine bora wangebaki wachunge ng`ombe za baba zao kijijini" ni maneno aliniambia mwalimu wa kike wa geography Olevel pale Kibaha sec.kisa kauliza swali sikumuelewa si unajua tena form one sie wa kijijini english ilikuwa majanga..baada ya kuelewa kizungu niliwatoa kamasi jamaa mpaka somo lake nikaongoza ila iliniuma sana siku ile.
 
Back
Top Bottom