KERO Walimu Nanyumbu tunadai stahiki za Uhamisho za tangu Mwaka 2023

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mmoja wa walimu waliopata uhamisho katika Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, mkoani Mtwara. Uhamisho wa kwanza ulifanyika mwezi Desemba 2023 kwenda shule mpya za Mkapa Wasichana Sekondari na Rukumbi Sekondari. Baadaye, mwezi Julai 2024, kulikuwa na uhamisho mwingine kwenda shule za Advanced Level ambazo ni Nangomba Sekondari na Nanyumbu Sekondari.

Pamoja na uhamisho huo, hadi sasa hatujalipwa kikamilifu stahiki zetu. Hata ile disturbance allowance tuliyolipwa haijakamilika, na bado kuna madai mengine muhimu kama ya wategemezi, usafiri wa mizigo, pamoja na subsistence allowance ambayo hatujalipwa kabisa.

Kinachosikitisha ni kwamba sasa tunaelekea mwaka wa nne tangu baadhi yetu tuhamishwe, lakini hakuna majibu ya kuridhisha kutoka kwa watendaji wa halmashauri. Kila tunapofuatilia tunaambiwa tusubiri, lakini hakuna hatua inayoonekana kuchukuliwa.

Hali hii inatukatisha tamaa sana, kwani tunatekeleza majukumu yetu kwa uadilifu lakini haki zetu za msingi hatupati. Tunaendelea kufanya kazi katika mazingira magumu bila stahiki zetu muhimu.

Tunaomba kupitia vyombo vya habari na mamlaka husika suala hili lifuatiliwe kwa karibu ili haki zetu zilipwe na matatizo haya yatatuliwe haraka. Tunahitaji msaada, kwa sababu kwa sasa hatuna pa kukimbilia.”

Pia soma ~ Naibu Waziri Qwaray: Waajiri wote lazima watenge bajeti ya kumlipa mtumishi pindi anapohama
 
Kwa Jinsi malalamiko yanavyoongezeka inaonesha Hali ni ngumu sana ya maisha
 
Hali basi ni ngumu Sana Kwa halmashauri, malalamiko ni mengi Sana. Poleni Sana watumishi.
 
Back
Top Bottom