Walimu naombeni ushauri kwa hili

Walimu naombeni ushauri kwa hili

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
5,950
Reaction score
11,295
Nilianza kazi mwaka 2008, 2011 nikaenda kusoma na ruhusa nilinyimwa nikatoroka kwenda Masomoni na mshahara ulikatwa.

Nimeripoti jana kwa DEO akadai nikaandike barua na isainiwe na Mkuu. Nikaenda kwa watu wa mishahara wakadai nimefutwa kwe Payroll.U

tumishi wakadai niende kwa mkurugenzi na nikafika ila mazungumzo tuliyafanya na DEO na muafaka ni kuandika Barua niliopewa kua nimerudi. Je waalimu wenzangu nitarudishwa kwe Payroll au nitafukuzwa kabisa?au itakuaje wapendwa waaalimu!
 
Hautafukuzwa ila itakuchukua muda kurudishwa kwenye payroll. cha msingi uwe mvumilivu huku ukiwafuatilia kwa sana. usiwe mjuaji maana wanaweza kukuhesabia utoro miaka yote uliyokuwa masomoni.
 
Huta fukuzwa ila usogope usumbufu,ila ungefanya utafiti kujua umetolewa lini kwenye payroll kwa kuangalia salary slip kwan kunauwezekano pesa zako wanazila hapo halmashaur
 
Itabidi kukomaa sana aisee kufutwa kazi sio rahisi lakn utahenyeka sana mpaka kurejeshwa kwenye payroll inabid uwe mpole usilete ujuaji...
 
  • Fuata maelekezo utakayopewa na TSD, TSD ndio wahusika katika hili.
  • Ofisi ya AFISA utumishi na DEO ni wamaliziajia wa maagizo yatayotoka TSD
  • Kwenye Pay Roll utarudishwa , ondoa shaka katika hilo
  • Ila utaanza kupokea mshahara wako kwa daraja lili lile la awali ulilokuwa nalo.
  • Itachukuwa muda kuweza kubadilishiwa ili kupata daraja jengine.
Nilianza kazi mwaka2008,2011 nikaenda kusoma na ruhusa nilinyimwa nikatoroka kwenda Masomoni na mshahara ulikatwa.Nimeripoti jana kwa DEO akadai nikaandike barua na isainiwe na Mkuu.Nikaenda kwa watu wa mishahara wakadai nimefutwa kwe Payroll.Utumishi wakadai niende kwa mkurugenzi na nikafika ila mazungumzo tuliyafanya na DEO na muafaka ni kuandika Barua niliopewa kua nimerudi.Je waalimu wenzangu nitarudishwa kwe Payroll au nitafukuzwa kabisa?au itakuaje wapendwa waaalimu!
 
Itachukua muda gani labda wapendwa
 
Back
Top Bottom