Walimu mliingia na vyeti vya kufoji? Mbona mnakandamizwa kama watu ambao hamjagusa hata darasa? Hebu tizama tofauti hii ya kutisha ya viwango vya mishahara kwa watumishi wa umma wa tz. Ajira mpya ngazi ya cheti: mwl 244,400/= afya 472,000/= kilimo/mifugo 959,400/= sheria 630,000/=. Ngazi ya Diploma: mwl 325,700/=, afya 682,000/=, kilimo/mifugo 1,133,600/=, sheria 871,500/=. Ngazi ya Degree. Mwl 469,200/=, afya 802,200/=, kilimo/mifugo 1,354,000/=, sheria 1,166,000/=. Kwanini walimu mnanyanyaswa hivi katika utumishi wa umma wa taifa moja lenye soko la bidhaa lililo na mfumuko wa bei wa kutisha? Kisa cha kuwadharau na kuwapa hela kiduchu ni nini? Eti sababu mpo wengi...hiyo siyo sababu. Walimu nawaombeni muungane msimame imara kudai ongezeko la mshahara kwa 50%. Msiwategemee hao viongozi wenu wa CWT au TUCTA, hao wanatumika kisiasa! Hamtakuja kufanikiwa kupitia cwt au tucta. Nawasilisha kwa uchungu mkubwa...maana mmekuwa watumwa ndani ya nchi yenu. Tena nyie ndo mnatumika na wanasiasa..kwnye uchaguzi, sensa etc. Kataeni kupuuzwa kwa vihela hivyo, mnakosa gani ktk nchi hii?