Walimu saba wafukuzwa kazi Baada ya kifo cha mwanafunzi wa miaka 12 aliyezama kisimani Shule ya Isenegeja

Walimu saba wafukuzwa kazi Baada ya kifo cha mwanafunzi wa miaka 12 aliyezama kisimani Shule ya Isenegeja

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Walimu saba kati ya 12 wa Shule ya Msingi Isenegeja, Kata ya Mwisi, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wameondolewa kazini kufuatia kifo cha mwanafunzi William Kapingu (12), aliyefariki dunia baada ya kuzama kisimani alipokuwa akichota maji kwa maagizo ya walimu.

Wakazi wa eneo hilo waliwakataa walimu hao, akiwemo mkuu wa shule, katika mkutano wa hadhara wakidai wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, jambo lililosababisha kifo cha mwanafunzi huyo.

Tukio hilo lilitokea Oktoba 13, 2025, ambapo inadaiwa walimu waliwatuma wanafunzi kuchota maji kwenye kisima chenye kina kirefu kilichopo umbali wa zaidi ya kilomita moja kutoka shuleni. Wakati wakichota maji, Kapingu alizama na kupoteza maisha.

Wananchi wamelalamika kuwa hakuna mwalimu aliyeshiriki kwenye mazishi ya mwanafunzi huyo, wala kutoa msaada wowote wa kusafirisha mwili au rambirambi kwa familia.
 
Inasikitisha sana.

Mtoto wa miaka 12 wa kumchotesha maji visimani!
Maji ni huduma ya Lazima shuleni, Serikali inaposhindwa kuwajibikia huduma hiyo, wazazi walipaswa kuwajibikia, nao wanaposhindwa kuwajibikia, inakuwa hakuna namna nyingine ila tu kutumia wanafunzi.

Lakini kuchota maji, kufagia, kulima, nk ni sehemu ya mafunzo pia shuleni. Mtoto wa miaka 12 hata nyumbani anafanyishwa kazi zote hizi. Hatulei mazezeta.

Kosa la walimu ni kuelekeza watoto kwenda sehemu hatari pasipo wao wenyewe kuwepo. Na kama walikuwepo ila walikosa maarifa, basi ni ajali tu na wakulaumiwa hasa ni Serikali.
 
Serikali iliyoshindwa kusogeza huduma maji shuleni hapo ifurushwe nayo maana ndio kiini cha tatizo.
Kungekuwa na maji shuleni, walimu wasingekuwatuma wanafunzi na marehemu asingekufa kwa kutumbukia kisimani.
Hakika.
Halafu kuna upuuzi Serikali inafanya katika ujenzi wa miundombinu ya vyoo mfano. Wanalazimisha kila Shule iwe na vyoo vya ku-flash, wenyewe wanaita vya kisasa, tena vyenye sink yenye elbow, sehemu ambayo hata maji ya kunywa ni shida. Hii inafanya wanafunzi wawe wanatjmia muda mwingi sana kuhangaikia maji, na kuvubua vyoo kujipaka kinyesi maana hawana vitendea kazi.
Vyoo vya shimo bado vina nafasi yake katika maeneo mengi.
 
Ila hii kazi🙆‍♂️
Yaan wanaonewaga kama makondoo tu

Sijaona kosa hapo la kufukuzwa hao walimu

Tatzo la kazi ya ualimu hata diwani anaweza kukufukuza kazi
 
Kwanini uwatume wanafunzi kuchota maji.umbali wa km 1 wakiwa peke yao
Suala la kusogeza huduma ya maji karibu na shule ni la mwalimu? Haya watoto wanatakiwa kula shuleni kutumia vyoo, hayo maji wachote walimu? Watoto kuchota maji huko wameanza leo? Ajari haina kinga na ajari haichagui haikuwa na haja ya kuchukua maamuzi ya haraka kiasi hicho.
 
Kwanini uwatume wanafunzi kuchota maji.umbali wa km 1 wakiwa peke yao
kukosekana kwa huduma ya maji shuleni kumechangia sana katika kifo cha mwanafunzi huyo. Hao wanakijiji ni kama mazezeta,wanawafukuzisha kazi walimu halafu swala linabaki palepale,hapo wamewakosesha watoto wengine haki ya kupata elimu bora,kwani mpaka wakaajiliwe walimu wengine miezi ipite,alafu pia tatizo la ukosefu wa maji litabaki palepale. Hapo wa kulaumiwa ni serikali kwa kushindwa kupeleka huduma ya maji shuleni ambayo huwa ni lazma na muhimu sana. Ningeishauri serikali hasa mkurugenzi wa wilaya ya igunga asiwafute kazi walimu hao bali awahamishe kwenda kwenye shule nyingine na ahakikishe kila shule inafikiwa na maji safi ya bombani. Kwani bila shaka mkoa wa tabora umepitiwa na mradi wa maji kutoka lake victoria au achimbe kisima kila shule za wilaya yake na tanzania nzima kwa ujumla. Pole kwa kumpoteza kiongozi wa kesho,pole kwa wazazi na walimu wote.
 
Hapo wa kulaumiwa Moja Kwa Moja ni serikali ya ccm imeshindwa kabisa kutatua changamoto za maji hasa kwenye huduma muhimu kama shule nk.
 
Back
Top Bottom