Mtumishiwetu
Senior Member
- Jul 13, 2022
- 196
- 346
Barua ya Wazi kwa Waziri wa TAMISEMI, Mhe Innocent Bashungwa
Sisi wananchi Bagamoyo ambao ni Wazazi wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Hassanal Damji iliyoko Bagamoyo tunayo masikitiko makubwa juu ya mazingira mabovu ya walimu wetu wanaofundisha kwenye shule hiyo ya Serikali.
Mazingira ya shule ni mabovu sana kwa walimu wetu kwani tunapozungunza sasa hivi walimu hawana ofisi yenye viti, meza, na shelf za kutunza nyaraka zao kwa muda mrefu.
Walimu wanakaa chini ya miti hivyo wanaposahihisha madaftari ya wanafunzi pia wanashindwa kuandaa masomo yao vizuri na kuifedhehesha taaluma ya ualimu ambayo ndio imekufikisha hapo ulipo Waziri wa Tamisemi Bashungwa na Waziri wa Elimu Prof Mkenda.
Walimu wetu hawana vyoo kwa sasa licha ya idadi kubwa ya Walimu lakini wana Matundu 3 tu Walimu wa kiume tundu 1 na walimu wa kike matundu 2 ya choo na kuwaletea usumbufu mkubwa sana walimu wetu.
Jambo la kusikitisha sana Serikali inaweza kujenga madarasa yenye hadhi kwa wanafunzi bila kuangalia ofisi za walimu zenye hadhi kulingana na taaluma zao.
Bahati mbaya sana Mbunge wetu tangu amechaguliwa hajawahi kufika Shuleni kujionea matatizo haya hivyo tumeona tuandike barua hii ili uweze kufika Shuleni na kujionea mwenyewe Mazingira ya shule yalivyo.
Wazazi tumelalamika sana kwa viongozi wetu wa Wilaya Madiwani, Mbunge wetu Mhe. Muharami Mkenge, Mkuu wa Wilaya, Zainab Issa juu ya Mazingira mabovu ya shule hii lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa za kuwasaidia walimu wetu kuboreshewa mazingira licha ya kazi ngumu wanayofanya.
Tumeona tukuandikie barua ya wazi kwako Waziri wa TAMISEMI ili usaidie kuifikia shule yetu maana haiko mbali ukitoka Dar es Salaam Bagamoyo sio mbali ili ufike uone kwa macho yako walimu wanavyolalilika.
Tuna imani na wewe ni Waziri mchapakazi na tunaamini suala hili utalichukua kwa uzito mkubwa ili kuwasaidia walimu wetu wa Shule ya Sekondari Hassanal Damji iliyoko Bagamoyo Mkoa wa Pwa
Sisi Wazazi wa wanafunzi
Hassanal Damji Sekondari
Bagamoyo, Pwani