Walimu toka Kenya na mustakabali wa elimu yetu

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Hivi karibuni kumekua na ombwe la kuajiri walimu toka nchi jirani ya kenya katika shule binafsi kwa mantiki ya kufundisha lugha ya kingereza kwa ufasaha.

Shule hizi zimekua zikiwapa ajira walimu si tu kutoka kenya bali pia na Uganda.

Naona hatari ya kuwaachia wageni maamuzi ya nini cha kuwafundisha watoto wetu darasani, huu ndo mwanzo wa kuuua elimu tuliyokua nayo kipindi cha nyuma.

Sisi hatukusoma hizo shule binafsi wala kufundishwa na walimu toka kenya au uganda lakini bado tuiweza kuandika na kuongea lugha ya kingereza kwa ufasaha kabisa.

Serikali iangalie utaratibu huu unaoendelea bila hivyo kuna hatari inakuja na muda si mrefu tutakuja juta wakati tumechelewa.
 
Mkuu mimi sioni tabu iko wapi. Shule zetu zinauhaba wa walimu, kwenda nchi jirani kutafuta suluhisho kuna tabu gani?
 
Ha ha ha ha ha we sema huna mpunga wa kulipia wanao sioni taabu watoto wetu wakifunzwa na waalimu toka Kenya au Uganda provided wanafuata mitaala yetu.

kama ni walimu kutoka Kenya halafu hawajui ni wabovu basi ni kweli kuna tatizo lakini kama ni walimu kutoka Kenya lakini ni wazuri ukifananisha na walimu wetu wa hapa Tanzania basi waendelee kuja tu wawafundishe wadogo zetu kiingereza
 
Ha ha ha ha ha we sema huna mpunga wa kulipia wanao sioni taabu watoto wetu wakifunzwa na waalimu toka Kenya au Uganda provided wanafuata mitaala yetu.
shughulisha ubongo wako kufikiria ya mbele zaidi ya haya niliyoaandika usiwe mpofu wa fikra, wapo walioelewa nilichomaanisha hapa, hatari ipo tena kubwa sana tutakuja jadili hapa siku moja
 
kweli kabisa elimu ya bongo tufundishane ssi kwa ssi elimu yetu to complicated hawawezi wagen
 
Ajira Wanachukua Wageni! Kama tunataka walimu wa kiingreza basi tuchukue wazungu, wakenya hawana kiingereza cha kuwafundsha watoto wetu. WATANZANIA TUNADHARAULIANA!
 
Mkuu mimi sioni tabu iko wapi. Shule zetu zinauhaba wa walimu, kwenda nchi jirani kutafuta suluhisho kuna tabu gani?

Mkuu hapa umepotoka. Walimu wapo ila wanadharaulika sana kuanzia jamii hadi serikali. Kuna haja gani yakuchukua walimu nje ya Nch wakati kila mwaka walimu wasiopungua 10000 wanagraduate!?
 
Ha ha ha ha ha we sema huna mpunga wa kulipia wanao sioni taabu watoto wetu wakifunzwa na waalimu toka Kenya au Uganda provided wanafuata mitaala yetu.

I.diot!! Kujua english sio sababu ya kuwapapatikia. Hata wewe unaweza kujua kuongea english ila ukawa na uelewa mdogo. Likewise kujua kuongea kiswahili sio sababu ya kuweza kukifundisha kiswahili!!
 
As long as hao walimu toka Kenya ama Uganda wana sifa za kufundisha sioni tatizo. Tena ikibidi wapewe ajira kwenye shule zetu za kata manake zina uhaba wa walimu
 
Mkuu hapa umepotoka. Walimu wapo ila wanadharaulika sana kuanzia jamii hadi serikali. Kuna haja gani yakuchukua walimu nje ya Nch wakati kila mwaka walimu wasiopungua 10000 wanagraduate!?

Mkuu, hivi umewahi kujiuliza kama wanagraduate walimu hao wengi kwanini bado kuna uhaba?
Kwani hao wakenya na waganda wanalipwa fedha gani?
Mimi nilisoma kozi tofauti na uwalimu nikakutana na watu wamemaliza ualimu na wako huko.
Walimu wenyewe wanatakiwa kupenda kazi yao halafu wajipange kupigania maslahi yao.
Je madaktari nao wakimbie taaluma waliosomea kwasababu ya maslahi?
 
Mkuu mimi sioni tabu iko wapi. Shule zetu zinauhaba wa walimu, kwenda nchi jirani kutafuta suluhisho kuna tabu gani?

Tabu ni kuwa wanaokuja si walimu bali wanaweza kuongea Kiingereza tu huku wakiwa sio professional teachers,Hatari yake ni kupoteza uwezo wa wanafunzi waliofundishika na badala yake watoto huwa wanategemea kuiba mitihani ili kuonekana wamefaulu kwa kiwango cha juu huku wakiwa na viwango vya chini sana kiuhalisia
 
Hapa sasa unazungumzia tatizo lingine kabisa..
Kwani idara ya ukaguzi inafanya shughuli gani mkuu?

Inabidi tuweke utaratibu wa ukaguzi hadi kwenye kutoa vibali vya kufanya kazi ya ualimu.

Ila nasisitiza kama walimu hapa hakuna bora tufungue milango waje kufanya kazi
 
Wakaguzi wanaweza kutembela shule moja baada ya miaka hata mitatu kupita,pia wanapewa bahasha mara wafikapo na kufanya waishie ofisi ya mkuu wa shule,walimu feki wanaendelea kusurvive na mchango wao ni mdogo sana kwenye kukuza elimu.
 
Mkuu, stick na issue moja tumalize! Sasa tena umerukia mambo ya rushwa!????
 
nadhani walimu wageni wanahitajika hapa nchini kunyanyua elimu
 
Mkuu nimekuelewa!
 
Ha ha ha ha ha we sema huna mpunga wa kulipia wanao sioni taabu watoto wetu wakifunzwa na waalimu toka Kenya au Uganda provided wanafuata mitaala yetu.

Sina hakika lakini nafikiri Arusha kuna waalimu wengi kutokk Kenya kulikomikoa mingine.wafundisha ktk shule xa binafsi ambao wanfaulisha vizuri kuliko shule za serikali.
kama ni kusoma wamesom kwao.nafikiri pengine kuna shida ktkt mfumo tunotumia kufundishia.
 
binafsi sipendi kabisa hii tabia. sababu kubwa ni moja, watoto watakuwa wanafundishwa itikadi za kiKenya au kiUganda. ni vizuri kwa nchi kama yetu kuwa na walimu wazalendo ili watoto wawe na doctrine za kitanzania kutoka kwa walimu wa kiTanzania. ni mtazamo wangu tu. nachukia kuona watoto wanajazwa mawazo kutoka nje. sidhani kama kuna walimu (wageni) ambao watatoa mifano inayoendana na mazingira ya Tanzania watakapokuwa wanafundisha masomo hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…