Toka naanza kusoma ,waalimu walitukaririsha neno "stomach" Kwa kushika tumbo kama moja ya maeneo ya nje ya mwili. Ukweli ni kwamba tumbo unaloweza kuligusa nje linaitwa "abdomen" na sehemu ya utupu ndani ambako kuna tumbo chakula yaani "stomach", ini yaani "liver" , bandama yaani "spleen" ,kongosho yaani "pancrease" ,utumbo mwembamba yaani "duodenum" ,utumbo Wa kati yaani "ileum" ,utumbo mpana yaani "colon" ,figo yaani "kidneys" na pia unaweza ukajimuisha kibofu cha mkojo yaani " urinary bladder".
Kwa mantiki hii wanapofundisha watoto waseme stomach wakishika tumbo si sahihi, wanakuwa wanataja kiungo kimoja kinachopatikana katika pango la tumbo yaani "abdominal cavity"
Kwa mantiki hii wanapofundisha watoto waseme stomach wakishika tumbo si sahihi, wanakuwa wanataja kiungo kimoja kinachopatikana katika pango la tumbo yaani "abdominal cavity"