Walimu tusikubalia taaluma yetu kuitwa wito

Joined
Mar 5, 2014
Posts
93
Reaction score
48
Ni unafiki wa hali ya juu kuuita ualimu wito katika karne hii, lazima tufike mahali ukweli uwekwe wazi hata kama unauma Ualimu ni taaluma na ndiyo maana zipo mada za sayansi ya ufundishaji na ujifunzaji "teaching pedagogy" leo waalimu wanalishwa sumu eti ualimu ni wito,hii ni zaidi ya kejeli mbona hawasemi siasa ni wito?

WITO "CALLING" Wanasiasa acheni upuuzi jaribuni kuwa wastaarabu hata kidogo juu ya hili maana hata na nyie mmepitia katika mikono ya waalimu.

Hakuna Mtanzania mjinga kiasi hicho leo hii, wabunge wanasinzia Dodoma, na kupewa sitting allowance, usafiri na mafuta ya gari plus ulinzi mwalimu anakomaa na chaki mnasema wito? ni yupi anayesomea taaluma ya kujitolea tu? Hata Yesu hakujitolea hivihivi tu alikufa msalabani kwa dhambi zetu ili tuokolewe na kwa maana hiyo neno "Wito"hapo halipo.

Mwalimu Nyerere aliwaainisha maadui wakuu watatu wa taifa hili na mmoja wapo huwa anaondolewa na walimu bora na si bora waalimu,wenye taaluma bora na sifa za ualimu na siyo "wito"kama mnavyodai ninaamini hakuna kitu kinachofanyika duniani bila maslahi yoyote yale "everything is value ladden"
Mwalimu kataa unafiki,kataa dharau kataa ualimu kudhalilishwa.
 
Jaribu kufuatilia history of education na hapo utagundua hii ni kazi ya wito au la!

"Usitumie neno wito kunyanyasa au kukataa majukumu"
 
Hivi wanaposema ualimu / udaktari au unesi (na kazi nyingi za huduma) ni wito wanamaanisha nini ?

Nadhani mkuu maana ya haya maneno ni kwamba kufanya hizi kazi ipasavyo lazima uwe na moyo wa kupenda kazi yako and to go an extra mile..., kujitolea beyond your job description ili kumweka sawa mwanafunzi asiyeelewa.., kumuhudumia mgonjwa aliye hoi na aliyekata tamaa hata kama upo off kazini au sio muda wa kazi.

In short kama unafanya hizi kazi sababu umekosa alternative au second choice basi you are in a wrong profession, sababu hizi kazi they need more than 100% hence wito (not everyone is cut to do them) na kuwa na cheti au mwalimu by profession does not make you MWALIMU
 
Ualimu ni taaluma kamili hakuna wito hapo...rejelea maana ya wito kwa undani wake
 
naomben mnisaidie hivi mwaka huu kuingia chuo cha uwalim ni kuanzia four ya ngapi hadi ya ngapi?
 
naomben mnisaidie hivi mwaka huu kuingia chuo cha uwalim ni kuanzia four ya ngapi hadi ya ngapi?

Acha kejeli wewe unauliza ni kuanzia four au mwisho ni point ngapi?that means unahisi ulimu ni mpaka uwe na four au?..acha utoto tupo waalimu wenye one na two huku siyo four unayoisema
 

Polisi ualimu magereza uhamiaji jwtz zima moto secta ya afya hizi ni kazi za wito kama unaona siyo wito kajaribu halafu utuambie kamshahara kadogo kazi kubwa kama nini
 
naomben mnisaidie hivi mwaka huu kuingia chuo cha uwalima ni kuanzia four ya ngapi hadi ya ngapi?
Umeuliza kwa kejeli,ila ni Ualimu na sio uwalimu. pia tambua ukiwa na vigezo vya kusoma ualimu ngazi ya cheti basi unakubalika kusomea ngazi ya cheti katika taaluma zingine nyingi(kama sio zote ) hata kwa diploma pia ni hivyo, zinazofanana na masomo yako. Katika ualimu kabla ya div 5. ilikuwa four ya 27 wakati taaluma zingine ukiwa tu na div four yoyote cheti unasoma.Ukitaka kulinganisha angalia level ya cheti kwa cheti, diploma kwa diploma utajua wanaosomea ualimu wana vigezo vikubwa kuliko fani zingine. fani zingine diploma hata ukiwa na zero form six unasoma kutumia matokeo ya form four lakini sio ualimu.
 
naomben mnisaidie hivi mwaka huu kuingia chuo cha uwalim ni kuanzia four ya ngapi hadi ya ngapi?

UALIMU ni WITO dada Jackline,sio KIMBILIO LA WAKOSEFU!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Acheni kudhalilisha fani za watu,umefeli halafu unataka kwenda ualimu inamaana hata 3 huna unataka kwenda ualimu,nakushauri hesabu una D ngapi ukasome CBE,huku sisi hatutaki watu wavivu.
 
Kutokana na hoja ya kuwa wengine wanasema ualim ni wito , wengine wanadai kuwa ni kazi maana wamesomea kama kada zingine.ebu tusaidiane walimu tujue tupo zama za wito au utendaj na wajibu.
 
ualimu ni wito , ikiwa umeingia kwa ajili ya kutoka ujue umeumia....
 
Konda naomba msaada nishushe wami darajani sitaki niende mpaka mwisho wa safari yangu kituoni kwa kuwa ualimu ni kazi bora kuliko nyingine ni mama wa kazi zingine na maadili
 
kiukweli ualimu ukiu tazama katika upande mmoja washilingi unaweza kusema ni wito pia ukasema ni kazi nzuri unapo waona walimu wa mjini wana enjoy yaan full bata .usije ukajaribu ualimu sio kazi vijijini walimu wanapata shida hakuna mfano,,kwanza mtandao hamna,maji shida,huduma duni,nyumba hakuna,walimu watatu wanafunzi 600. na serikali ipo kimya,kifupi huwez kumkuta mtoto wa kiongozi waserikalini ni mwalimu,labda mjini.ULIZA ALIYE KUWA NAIBU WAZIRI WA ELIMU,PHILIPO MLUGO ,kwao kukoje? ukipelekwa huko sawa na jela.sitaki ualimu mimi bora nikawe mlinzi mjini.
 
ualimu si wito bali ni kiitikio...
ukipangwa nakahuga hakuna kubisha unaenda bila ubishi...

wito unakuja pale mambo ya kijijini yakizidi..
 



Nimependa sana ufafanuzi wako, wewe umeielewa vema dhana ya wito "intrisic motive"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…