A
Anonymous
Guest
Sisi walimu wa ajira mpya wa mwaka wa fedha 2025/2026, tulioajiriwa katika kipindi cha siku 100 za Mheshimiwa Rais, tunaomba mamlaka husika, hususan Ofisi ya Rais - TAMISEMI, isikilize na kutatua changamoto ya kutolipwa fedha zetu za kujikimu.
Hadi sasa, walimu wengi katika halmashauri mbalimbali bado hatujapokea malipo hayo, ilhali wenzetu wa sekta ya afya, ambao tuliingia kazini katika kipindi hicho hicho, tayari wameanza kulipwa stahiki zao. Hali hii inaleta hisia za kutokuwepo kwa usawa katika kuwahudumia watumishi wa umma wenye hadhi sawa ya ajira.
Tunaomba Ofisi ya Rais - TAMISEMI na mamlaka nyingine zinazohusika zitoe ufafanuzi kuhusu lini walimu wa ajira mpya wa mwezi Januari 2026 tutalipwa fedha zetu za kujikimu. Tunaamini kuwa stahiki hizi ni haki yetu na tunatarajia zitalipwa kwa wakati ili kutuwezesha kutekeleza majukumu yetu kwa utulivu na ufanisi.
Tunawasilisha ombi hili kwa heshima na matumaini kwamba litasikilizwa na kufanyiwa kazi kwa wakati.