KERO Walimu wa ajira mpya kutoka Babati Vijijini hatujalipwa fedha zetu za kujikimu

KERO Walimu wa ajira mpya kutoka Babati Vijijini hatujalipwa fedha zetu za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Walimu tulioajiriwa mwaka 2025/2026 katika Wilaya ya Babati Vijijini tunaomba kuwasilisha kero ya kutolipwa fedha zetu za kujikimu tangu tulipoanza kazi mwezi Februari.

Tumekuwa tukifuatilia suala hili, lakini kila tunapouliza tunaelezwa kuwa fedha bado hazijaingia katika halmashauri.

Hadi sasa hatujapewa taarifa ya wazi kuhusu lini tutalipwa fedha hizo, jambo ambalo linatuweka katika hali ya sintofahamu na changamoto za kifedha.

Tunaomba TAMISEMI na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Vijijini ulifanyie kazi suala hili na kutupa taarifa kuhusu hatma ya malipo yetu na muda tunaoweza kuyatarajia.
 
Back
Top Bottom