Walimu wa arts jiandaeni kisaikolojia

Mimi nimepangiwa shule fulani hapa Geita nimepewa form two geog. Vpnd 3 kwa wiki yaani dk 120 tgts in



acha kutuaibisha mkuu. geig ina vipindi 4 kwa week kila darasa hyo shule kama wameweka 3 mwambie mtaaluma aangalie muongozo kwenye muhtasari aongeze hicho kipindi kimoja
 
Kwa wastani mwalimu anatakiwa afundishe mkondo mmoja tu na asizidi vipindi viwili kwa week ili awe effective. Suala la kuwalundikia walimu vipindi thelathini limeonekana kuwa ndio utaratibu alhali tunaua efficiency inayochangia kushuka kwa elimu.

Kuwa na vipindi vichache na darasa la wanafunzi wachache pia kunapunguza mzigo wa usahihishaji, kusimamia kazi na mazoezi ya wanafunzi darasani, kuwa na mahusiano na kuwafahamu vizuri wanafunzi wako n.k.

Unayesema wajiandae kisaikolojia nikwambie tu wewe ndo umeshaathirika kisaikolojia. Ualimu si kuwa na vipindi 30-40. Kwa kazi alizonazo mwalimu (hasa katika hizi level za secondary) anastahili hata kufundisha darasa moja tu.

Nikupe mfano wa jinsi Universities kulivyo ambako kuna baadhi ya course wahadhiri hufundisha kwenye maeneo waliyobobea tu!

Kuajiriwa kwa walimu wa arts hakuwezi kuisha alhali bado tuna teacher-student ratio ya 1/70-1/100>!!!
 
Bora huko huku kuna shule zimejaa arts balaa mf sec 1 ipo ludewa walimu wanao hitajika ni 19 tu ila wapo 24 na kati ya hao 22 ni arts.
 

kwa wastan minimum ni 24 na maximum ni 28 vipindi!
 

Yaah! ni kweli bhana,sasa hivi walimu wa sayansi ndo wapo sokoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…