Kwa wastani mwalimu anatakiwa afundishe mkondo mmoja tu na asizidi vipindi viwili kwa week ili awe effective. Suala la kuwalundikia walimu vipindi thelathini limeonekana kuwa ndio utaratibu alhali tunaua efficiency inayochangia kushuka kwa elimu.
Kuwa na vipindi vichache na darasa la wanafunzi wachache pia kunapunguza mzigo wa usahihishaji, kusimamia kazi na mazoezi ya wanafunzi darasani, kuwa na mahusiano na kuwafahamu vizuri wanafunzi wako n.k.
Unayesema wajiandae kisaikolojia nikwambie tu wewe ndo umeshaathirika kisaikolojia. Ualimu si kuwa na vipindi 30-40. Kwa kazi alizonazo mwalimu (hasa katika hizi level za secondary) anastahili hata kufundisha darasa moja tu.
Nikupe mfano wa jinsi Universities kulivyo ambako kuna baadhi ya course wahadhiri hufundisha kwenye maeneo waliyobobea tu!
Kuajiriwa kwa walimu wa arts hakuwezi kuisha alhali bado tuna teacher-student ratio ya 1/70-1/100>!!!