Walimu wa halmashauri ya wilaya chato hili mlikatae kwa nguvu.

Walimu wa halmashauri ya wilaya chato hili mlikatae kwa nguvu.

Luraja

Member
Joined
Oct 15, 2012
Posts
27
Reaction score
4
Kweli adui wa mwalimu ni mwalimu.Hapa Chato maafisa elimu ambao kitaaluma ni walimu ndiyo wanakuwa wa kwanza kuwakandamiza walimu.Ni hivi karibuni maafisa elimu hawa wameagiza tena kwa lazima kwamba walimu wote wachangie madawati.Kinachosikitaisha mwalimu anachangia maendeleo kila mwezi kupitia kodi lakini kuna wafanyabiashara wengi ambao hata kodi hawatoi hata kama wanatoa ni kidogo lakini wao hawaambiwi kuchangia madawati.Hivi serikali inawaona walimu ni wanyonge kiasi hiki .Hivi chama cha walimu wilayani Chato hili mnalijua na kama mnalijua mmechukua hatua gani? Walimu hamkeni hacha woga pingine dhuluma hii ya waziwazi. Onyo kwa serikali iliyoko madarakani kuweni makini na viongozi hawa mbubu ambao wanatoa maamuzi ya ajabu vinginevyo mpaka inafika 2015 mtakuwa na kazi ngumu sana.
 
Hapo watakuwa wanaibiwa.Hilo si jukumu la walimu bali wazazi na wadau wengine kwa makubaliano maalum
Chama cha walimu kichukue mkondo wake kutetea wanachama wake.
 
Back
Top Bottom