Walimu wa kisasa kwaya za ibada za kikatoliki wanaua ladha halisi ya ibada za kikatoliki

Walimu wa kisasa kwaya za ibada za kikatoliki wanaua ladha halisi ya ibada za kikatoliki

"nimetafakari habari zako,nami nashindwa kuelewa kabisa,
Binadamu angenipa neema, kesho angechoka kunipa zaidi,
Lakini wewe hauna kikomo,wala mvua yako haina masika.
Bwanaaa wanyesha mvua, bwanaa kwa walio jangwani,
Bwanaaa wawasha jua,
Bwanaaa mpaka baharini,
bwana kweli wewe ni mwema sana.
Nitasiiiimulia nchi..Yesu Ni mwema Yesu Ni mwema.
Nitahuuubiri vijiji, Yesu ni mwema Yesu ni mwema."
Huu ni wa kizamani au wa kisasa wakuu?
 
Kitambo sana amekuwa akishutumiwa yeye na wenzake kama Gabriel Mkude, nk kutunga baadhi ya nyimbo zenye maudhui tofauti na zile zilizo zoeleka ndani ya Kanisa. Nothing more.
Hayo maudhui tofauti ni yapi mkuu?
Labda uniambie "mahadhi" ndio baadhi ya watu wanaona imekuwa tofauti!
...ninachofahamu Kuna nyimbo baadhi za hao watunzi Zina "mahadhi" ya nyimbo za dhehebu flani hivi ambalo hawasali jumapili, na nyingine kuwa na mapigo ambayo hayajazoeleka!
...binafsi niseme kazi ya utunzi si rahisi Kama wengi wanavyofikiria, kumponda mtunzi ni kumkosesha heshima yake hasa Kwa mtu ambaye hajui mziki mtakatifu!

Nipo kwenye hiyo field, naelewa changamoto zake!!
 
Kweli kabsa mfano zile nyimbo za xmass au Pasaka zilikuwa za hisia sana hadi raha, ila siku hizi sifa nyingi wana badilisha badilisha melody washenzi hawa
 
Zamani ilikuwa kwaya za kiibada zinavutia na kusisimua lakini wamekuja vijana wa hovyo wanajiita walimu wa kwaya yaaji Wana edit kila kitu mwisho wa siku kwaya za ibada hazigusi mioyo na kusisimua, ilikuwa kawaida mwanakwaya wa Bukoba kuimba kwaya Mtwara bila shidaa yoyote ila sasa ni ngumu...

Yamebaki majimbo machache yaliyotunza kwaya halisi za ibada za kikatoliki, hapa nilipongeze Jimbo la Bukoba na majimbo karibu yote ya kagera.

USHAURI: Naishauri TEC kuhakikisha wanadhibiti kirusi cha uharibifu wa kwaya halisi za ibada za kikatoliki,siyo kila kitu kiwe cha kisasa hii itakuwa vurugu kanisani na kutukosesha Iadha tam na muruaaaa ya ukatoliki.

Sasa hivi hata mapadri wa kisasa hawana ladha kwenye kuimba injili mpaka mtu unahisi unapaa mbinguni.

Mapadri wa zamani walikuwa na vionjo bwana wawapo madhabahuni mpaka tukawa tunavutiwa kuwa mapadri
Fvck religion

Christians are even worse
 
Hayo maudhui tofauti ni yapi mkuu?
Labda uniambie "mahadhi" ndio baadhi ya watu wanaona imekuwa tofauti!
...ninachofahamu Kuna nyimbo baadhi za hao watunzi Zina "mahadhi" ya nyimbo za dhehebu flani hivi ambalo hawasali jumapili, na nyingine kuwa na mapigo ambayo hayajazoeleka!
...binafsi niseme kazi ya utunzi si rahisi Kama wengi wanavyofikiria, kumponda mtunzi ni kumkosesha heshima yake hasa Kwa mtu ambaye hajui mziki mtakatifu!

Nipo kwenye hiyo field, naelewa changamoto zake!!
Bahati nzuri kwa upande wangu sina tatizo na hao watunzi. Kwa sababu natambua fika huo ni ununifu wao, na wala sioni kama ni tatizo. Ni baadhi tu ya waumini ndiyo wanawachukulia tofauti. Na mimi si mmoja wa hao waumini.
 
Mkuu huo ni uhafidhina,kubali mabadiliko yenye lengo jema.
Lengo jema???? 😵 Ibada ya Misa Takatifu inatakiwa iwe ni Shirikishi na sio ya kikundi cha kwaya au "Show" fulani. Kwaya izingatie kuwawezesha waumini kushiriki na kusali kikamilifu zaidi na kwa Uchaji kwenye Ibada.
 
Conservatism.............
Hata zamani ibada zilikuwa kilatini..
 
Matumizi ya kinanda Cha Technics U60 kwenye ibada nacho kimechangia kuhamasisha matumizi ya hizo nyimbo za mapambio za kizazi kipya
Kwani Kinanda kina kosa gani mkuu? Kwani ni lazima Mtumiaji/Mpigaji kinanda atumie kila function iliyo kwenye kinanda hicho? Functions nyingine sio kwa ajili ya matumizi ya kanisani/Ibada bali ni kwa ajili ya kwenye Jazz bands. Kama mpigaji kinanda hicho hawezi kutumia manual setting buttons au inbuilt computer setting kupata mlio mzuri wa kanisani ikiwa ni pamoja na kuchagua ngoma stahiki, hilo sio kosa la kinanda bali ni la mtumiaji.
 
No offense, ila wazee mnahisig kila kitu inabidi kiwe kama zamani 😂
Jueni dunia inabadilika, hizo nyimbo za kucopy ambapo tune inakuwa moja Tz nzima zama zake zishapita, kubalin kataenj ila hatutorudi huko tena
Mwe, mwe, mweee! Kumbukeni (esp. nyie walimu wa kwaya); hakuna Mungu wa kizamani na Mungu wa kisasa. Hapo ndipo mnapobweteka na kukosea sana. Kwani mtapungukiwa na nini kama mkiziboresha zile nyimbo za zamani zenye tune moja kwa kuziwekea soprano, alto, tenor na bass? Hivi huwa nyie mnajisikiaje waumini wenzenu wanapokaa kimya tuu kuwasikiliza mnapoimba halafu mwisho wa Ibada wanawasema/wanawajadili huko nje??
 
No offense, ila wazee mnahisig kila kitu inabidi kiwe kama zamani [emoji23]
Jueni dunia inabadilika, hizo nyimbo za kucopy ambapo tune inakuwa moja Tz nzima zama zake zishapita, kubalin kataenj ila hatutorudi huko tena
Eti watu wanataka kusikia zile tune za wababu na wabibi za kilatini...daah!!!
 
"nimetafakari habari zako,nami nashindwa kuelewa kabisa,
Binadamu angenipa neema, kesho angechoka kunipa zaidi,
Lakini wewe hauna kikomo,wala mvua yako haina masika.
Bwanaaa wanyesha mvua, bwanaa kwa walio jangwani,
Bwanaaa wawasha jua,
Bwanaaa mpaka baharini,
bwana kweli wewe ni mwema sana.
Nitasiiiimulia nchi..Yesu Ni mwema Yesu Ni mwema.
Nitahuuubiri vijiji, Yesu ni mwema Yesu ni mwema."
Huu ni wa kizamani au wa kisasa wakuu?
Nyimbo za Kikatoliki ni sala. Sala yaweza kuwa Kusifu, Majuto, Maombi, Kushukuru n.k. Vyote hivyo vinapatikana ndani ya Biblia e.g. Zaburi n.k. Ndo mana kila dominika inayo Antifona ya kuingia, Zaburi/wimbo wa katikati na shangilio na inaoneshwa vimetoka wapi.
Je, Huo wimbo hapo juu 👆 👆 unakidhi vigezo hivyo? Hoja ya wa-kizamani au wa-kisasa haina mashiko sana kwani ni swala la muda tu. Hata hizo zinazoitwa ni za kizamani kuna wakati zilikuwa ni za kisasa (ref. Mzee = kijana wa zamani).
Nyimbo za kuhamasisha e.g. Kutoa sadaka, Kushiriki komunio(kwenda Kupokea)zisitufanye Wakatoliki tuache ile desturi njema ya kujitambulisha kwa "Nyimbo za Kikatoliki"
Sipingani na uwepo wa nyimbo "zilizochangamka", zenye "mguso" na Hamasa ya Ki-injili bali nashauri tusigeuze Ibada ya kanisani ifanane-fanane na Disco.
 
Kanisa

Kanisa linajengwa na wenye moyo! Ukiona vyaelea ujue vimeundwa! Shida yng ni hawa walimu wa hovyo wanaobadili ladha ya kale ya kwaya zetu za ibada
Bahati mbaya
Ndo imeisha hiyo mabadiriko ndo yanaendelea
 
Bahati mbaya
Ndo imeisha hiyo mabadiriko ndo yanaendelea
Na kwa Bahati mbaya hiyo hiyo ndo siku hizi Tunashuhudia uwepo wa Kwaya zilizosheheni kila aina ya kero, fujo, ubabaishaji, kiburi, majigambo n.k. na zinasahau kwamba ibada za Misa n.k. zinaweza kuendelea vizuri tuu hata bila ya kuwepo kwa Kwaya.
 
Back
Top Bottom