ngara23
JF-Expert Member
- Aug 31, 2019
- 9,091
- 21,087
Nilipe pesa nikufundishe kiswahiliSawa hayo ni mawazo yako.
Naona kiswahili hukijui
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilipe pesa nikufundishe kiswahiliSawa hayo ni mawazo yako.
Ndo ninapopata maswali, walimu wa kiswahili wanakwama wapi kurekebisha hili!?.Matatizo ya l na r, sehemu ya kuweka na kutoweka h, z na dh ni mengi sana hata hapa JF.
Mimi nikiona mtu anaandika hivyo picha ninahoipata ni kuwa huyu hana elimu na aghalabu sitaweza kujadiliana naye kimantiki.
Haya matatizo ni mengi sana hata hapa JF mpaka yanazoeleka na unayekosoa ndiye unaonekana tatizo.
😀Nimecheka bila kupenda, eti leema.Binafsi nililiona hilo tatizo kwa wanangu, nikaongea na mwalimu mkuu, sikuona mabadiliko. Nimeamua kabisa kuwa mwalimu, siwezi kuvumilia kuona mwanangu anaongea kiswahili kibovu.
Mtoto anakuja nyumbani anasema "baba leo lafiki angu leema akuja shule"
Nakuwa mwalimu hakuna namna.
Serikali inaigiza kuwalipa mishahara walimu, na walimu wanaigiza kufundisha.Ndo ninapopata maswali, walimu wa kiswahili wanakwama wapi kurekebisha hili!?.
Kwani wanafunzi kuwa wengi imeanza Leo!?. Wakati wetu tulikuwa A mpka E na tulifundishwa tukaelewa.Serikali inaigiza kuwalipa mishahara walimu, na walimu wanaigiza kufundisha.
Jamii yetu ina matatizo mengi sana, huwezi kuwaachia kila lawama walimu.
Mwalimu ana darasa lenye wanafunzi 100, unafikiri ataweza kuwafuatilia wote hao?
Wanafunzi wenyewe wanamuheshimu mwalimu au wanamuona ni kidampa tu aliyeshindwa maisha ukimlinganisha na Konde Boy na Diamond Platnumz?
Siku hizo jamii haikuendeshwa kwa kila kitu kuwa "pesa mbele" kama leo.Kwani wanafunzi kuwa wengi imeanza Leo!?. Wakati wetu tulikuwa A mpka E na tulifundishwa tukaelewa.
Walimu wa sasa hawafundishi kwa mapenzi, wanafundisha ilimradi siku ziende.
Ni kweli hapo umenena, hakuna wito tena kama zamani.Siku hizo jamii haikuendeshwa kwa kila kitu kuwa "pesa mbele" kama leo.
Walimu waliaminishwa kuwa wanafanya "kazi ya wito".
Na wengi waliamini hilo. Na ilikuwa rahisi kuamini kwa sababu jamii ilikuwa inaenda kijamaa zaidi, unaweza kuwa hulipwi mshahara mkubwa lakini gharama za maisha ziko chini, hospitali za serikali bure, watu hawaishi kwa mashindano, tofauti kati ya masikini na tajiri si kubwa sana, jamii ilikuwa haijakuwa tight sana kwenye ubepari.
Mimi nimesoma na mtoto wa rais darasa moja shule ya msingi. Hawa watoto wa mawaziri, wakurugenzi ndio usiseme. Nchi haikuwa na madaraja ya wazi.
Siku hizi kila kitu ni pesa, tofauti ya masikini na tajiri ni kubwa, jamii inaenda kibepari zaidi, nchi ina madaraja ya wazi, utamuaminisha vipi mwalimu kwamba ualimu ni kazi ya wito?
Ilikuwa sh 5 unaenda nayo shule unakula na kubakiza.Ni kweli hapo umenena, hakuna wito tena kama zamani.
Vitu vilikuwa vinauzwa sh. 5. Sasa hivi elfu 10 inatumika siku 1 😢
Mimi nishakula muhogo wa kukaanga wa shilingi moja.mimi nimeikuta sh. 5, shule ilikuwa tunaenda na sh. 20. Senti sikuzikuta wakati huo
Umekula chumvi kumbe. Ila mimi naona suluhu nasi tuwe mabalozi wa lugha yetu pendwa ya kiswahili. Tuwe tunaweka mada angalau kwa week mara Moja za matamshi na maandishi sahihi ya kiswahili, huenda tukasaidia kupunguza tatizo. Wasojua huenda nao wakapata mwanga fulani.Mimi nishakula muhogo wa kukaanga wa shilingi moja.
Kuna siku niliokota shilingi 60 uwanja wa mpira, mwaka 1982. Siku ile ilikuwa kama sherehe nilijiona bonge la tajiri.
Nafikiri siku zile hata noti ya shilingi 1,000 ilikuwa haijachapishwa bado.
Mimi kwa kuanzia sasa kila ninapoona mtu anaharibu nakosoa kama Mzee Kifimbocheza.Umekula chumvi kumbe. Ila mimi naona suluhu nasi tuwe mabalozi wa lugha yetu pendwa ya kiswahili. Tuwe tunaweka mada angalau kwa week mara Moja za matamshi na maandishi sahihi ya kiswahili, huenda tukasaidia kupunguza tatizo. Wasojua huenda nao wakapata mwanga fulani.